Nafasi Ya Matangazo

February 19, 2015

Mnamo tarehe 19/02/2015 majira ya saa 13:15hrs huko eneo la Vikonje Kata ya Mtumba Barabara ya Dodoma – Morogoro, Magari mawili yamegongana uso kwa uso na kusababisha vifo vya watu wawili na majeruhi 45.



Ajali hiyo imehusisha Basi lenye namba za usajili T. 663 AXL aina ya SCANIA Kampuni ya KIDIA ONE lililokuwa litokea Dar es Salaam kwenda Mwanza likiendeshwa na ADAM s/o ROBERT, 38yrs, kabila Mnyaturu, mkazi wa Tegeta Dar es Salaam, liligongana uso kwa uso na Lori namba T.469 CFG Scania lenye Tellar T. 756 AZX.



Watu wawili walifariki dunia papo hapo ambao ni dereva wa Lori aitwaye FADHILI S/O HAMIDU SAIDI miaka 36, Kabila Msukuma na utingo wa Bus aliyehafamika kwa jina la CHOGO S/O CHIGUNDA, miaka 30, Kabila Muha wote wakazi wa Dar es Salaam.



Watu waliojeruhiwa ni 45 kati yao 33 ni wanaume na 12 ni wanawake; wengine wametibiwa na kuruhusiwa. Waliolazwa ni 24 kati yao wanaume ni 17 na wanawake ni 7.



Chanzo cha ajali ni dereva wa Bus Kushindwa kuchukua tahadhali wakati wa kulipita gari lingine “over take”, na kusababisha ajali hiyo.



Kamanda wa Poliisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi D.A. Misime – SACP ametoa wito kwa madereva kuwa na udereva wenye tahadhali na kuzingatia sheria za usalama barabarani, kwani dereva huyu wa basi angezingatia hilo ajali hii haingetokea na hatakama ingetokea madhara yake hayangekua makubwa kiasi hicho. 

Imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi MISIME D.A (SACP).
Posted by MROKI On Thursday, February 19, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo