Afisa Mahusiano
wa Airtel Tanzania, Jane Matinde (wa pili kushoto) akiongelea umuhimu wa
promosheni ya Mimi ni Bingwa muda mfupi baada ya kukabidhi shilingi
milioni moja kwa baadhi ya washindi wa promosheni hiyo (waliopo
pichani). Kushoto ni Bw. Ramdhani Wefa, Kulia ni Philemon Nathaniel
Mgaya akifuatiwa na Bw. Msemwa Makuzi ambaye pia ni mshindi wa tiketi na
wote wakiwa wanatokea Dar es salaam.
*******
Wakati
Kampuni ya mitandao ya simu za mkononi ya Airtel ikisubiria kuchezesha
droo kubwa ya shilingi Milioni 50 kupitia promosheni ya Mimi ni Bingwa,
baadhi ya washindi waliokwishapatikana wamejitokeza wakiisifia kampuni
hiyo kwa kuratibu promosheni zenye kulenga maendeleo kwa watanzania
walio wengi nchini.
Washindi
hao wameainisha hayo muda mfupi baada ya kukabidhiwa pesa zao mapema
wiki hii kwenye ofisi za makao makuu ya Airtel ziilizopo Morocco jijini
Dar es salaam.
Washindi
hao wamedai kuwa mara nyingi watu huwa hawaamini promosheni
zinazoendeshwa na kampuni ya simu kama Airtel na hivyo kujikuta wakibaki
nyuma kwa kuogopa kuthubutu.
“Mi
binafsi sikuwahi kumuambia mke wangu kwamba nashiriki kwenye promosheni
ya Mimi ni Bingwa sababu huwa akijua nashiriki ananikasirikia na kusema
nina matumizi mabaya ya pesa, lakini leo nimeibuka mshindi wa shilingi
milioni moja yeye akishuhudia na vilevile nimeshinda tiketi ya kwenda
kushuhudia mechi ya Manchester United kwenye uwanja wa Old Trafford,”
alisema mshindi huyo Bw. Msemwa Makuzi mkazi wa Dar es salaam.
Mshindi
huyo aliendelea kwa kusema, kwa hali ya kawaida ilikuwa ni ngumu
kuamini kwamba ameshinda shilingi milioni Moja na tiketi ya kwenda
nchini Uingereza kushuhudia mechi ya Manchester United kwenye uwanja wa
Old Trafford.
“Kweli
mimi kama mtu mwingine yeyote wa kawaida iliniwia vigumu kuamini kwamba
nimeibuka mshindi wa pesa hizo na tiketi. Na imenichukua muda kuamini
mpaka sasa baada ya kukabidhiwa hizi milioni moja ndo naamini kweli mimi
ni mshindi,” alimalizia Bw. Makuzi.
Aidha
washindi wengine wamewaasa wananchi kote nchini kujitokeza kwa wingi
katika promosheni hiyo kwani ina manufaa makubwa kwa maendeleo ya mtu
binafsi na taifa zima.
“Kwa
kweli mi nawaambia watanzania wenzangu wasidhani hivi vitu ni masihara,
watu wanashinda kweli na maisha yao yanabadilika kupitia hizi pesa
tunazopewa. Mimi hapa naiwinda hiyo milioni 50 kwani nina uhakika
nikishinda nitakuwa nimesahau kabisa umasikini,” alisema Ramadhani Wefa
ambaye ni mshindi wa milioni moja kutoka Kinondoni jijini Dar es salaam.
Kwa
upande wake Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde alisema
bado Airtel inatambua na itaendelea kutambua umuhimu wa wateja wake
hivyo haina budi kuhakikisha inatoa huduma bora na zenye manufaa kwa
wananchi wote kiujumla.
“Airtel
inaelewa fika kuwa wateja ndio kiini cha maendeleo ya kampuni hiyo na
hivyo inajitahidi kuhakikisha inatoa huduma bora za kuwanufaisha wateja
wake na kuleta maendeleo kwa taifa zima kiujumla,” alisema Jane.
0 comments:
Post a Comment