Nafasi Ya Matangazo

June 21, 2013

Tamasha la muziki wa dansi linalojumuisha bendi za zamani na za kisasa lijulikanalo kama raha za jana na leo ambapo jumla ya bendi sita zitapanda jukwaa moja kuonyeshana umwamba nani zaidi katika kukonga nyoyo za mashabiki siku hiyo. 
 
Waandaji wa tamasha hilo ambao ni Yuneda Entertainment wasema dhumuni la tamasha hilo ni kukutanisha radha ya muziki wa dansi ya kale na ya kisasa katika jukwaa moja ikiambatana na kuwaliwaza watoto waishio bila wazazi kwa kula nao, kucheza na kuwakumbuka wanamuziki wa dansi waliotangulia mbele ya haki. 
 
Akiongea na mwandishi wa habari hizi mratibu wa Tamasha hilo Kahabi Ng’wendesha amesema kuwa tamasha hilo litajumuisha bendi sita za muziki wa dansi nchini Tanzania ikiwemo bendi nne za muziki wa dansi wakongwe na bendi mbili za muziki wa dansi kizazi kipya.
 
 Bwana Kahabi akizitaja bendi hizo kuwa ni Sikinde, Msondo ngoma ,Twanga pepeta,Mashujaa musica,King kiki na Hamza kalala. Tamasha la Raha za jana na leo litafanyika siku ya jumamosi tarehe 6 mwezi wa saba katika viwanja vya chuo cha posta mkabala na chuo cha ustawi wa jamii vilivyopo jijini Dar es salaam ampapo milango ya uwanja itakuwa wazi kuanzia saa tano asubuhi hadi majogoo. 
 
Akitangaza vingilio vya siku hiyo Bwana Kahabi alisema kuwa watoto wataingia bure kabisa kuanzia saa tano hadi saa kumi na mbili ambapo watashiriki katika michezo na watoto wenzao waishio bila ya wazazi ikiwa ni fursa ingine kujumuika pamoja katika michezo mbalimbali. 
 
Pia kwa upande wa wakubwa watatozwa tshs 8000 tu mlangoni ambapo vinywaji na nyama choma zitapatikana ndani ya uwanja kwa muda wote kwa bei ya kawaida kabisa. 
 
Wito umetolewa kwa wazazi kuwaleta watoto wao siku hiyo ya tamasha la Raha za jana na leo ili wajumuike na watoto wenzao katika michezo mbalimbali,pia zawadi ndogondogo zitatolewa kwa watoto watakaonesha vipaji katika fani mbalimbali.
Posted by MROKI On Friday, June 21, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo