Nafasi Ya Matangazo

September 02, 2012

Redd’s Miss Kanda ya Mashariki 2012, Rose Lucas akiwa ni mwenye furaha baada ya kutajwa kuwa mshindi na kujinyakulia taji hilo baada ya kuwashinda warembo wengine 11 katika kinyanganyiro hicho cha aina yake.
Redd’s Miss Kanda ya Mashariki 2012, Rose Lucas katikati akipunga mkono kwa furaha akiwa na mashindi wa pili Irine Veda (kulia) na Mshindi wa tatu Joyce Baluhi mara baada ya warembo hao kutangazwa kuwa washindi wa shindano hilo lililofanyika mjini Morogoro usiku wa Septemba Septemba 1, mwaka huu. Warembo hawa wote watashiriki shindano la Redd’s Miss Tanzania 2012 baadae mwaka huu.
 
Washiriki wa Shindano la Urembo la Redd’s Miss Kanda ya Mashariki 2012 waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutajwa kufanikiwa kupita katikia hatua hiyo. Kutoka kushoto ni 6. Zuhura Gora,
7. Irene Veda, 4. Salvina Kibona, 9. Rose Lucas na 5. Joyce Baluhi.
Warembo wa Redds Miss Kanda ya Mashariki wakicheza show kali ya ufunguzi wa shindano lao lililofanyika Hotel ya Nashera Mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo.
Wandaaji wa mashindano ya Mikoa iliyoleta washiriki wa Miss Kanda ya Mashariki wakitambiana huku Mwandaaji wa Mkoa wa Lindi, Ramadhan Shaha (katikati) akionesha ishara ya ushindi aitumiayo mkiambiaji wa Kimataifa wa Jamaika Bolt. Shaha alifanikiwa kutoa mshindi wa pili wa mashindano hayo. Wengine kushoto ni Mwandaaji wa Mtwara, Rajab Mchata, Mwandaaji wa Morogoro, Frank Ezekiel na kulia kabisa ni Mama Mchata.
mrembo katika vazi la Ubunifu

Warembo wakirusha kete yao ya pili kwa kivazi cha ufukweni, katika harakati za kutafuta point mbele ya majaji.


Warembo wa Miss Tanzania 2010, Miss tanzania 2010 akiwa na mrembo mwenzake katika shindano hilo.
wadau wa Sanaa ya Urembo nao walikuwepo
 Mwandaaji wa Miss Mara, Godson Mukama akiwa na Miss Mara wa 2011
 Bondia Francis Cheka (kulia) akiwa na Mkali wa Rymes Afande Sele nao walishuhudia shindano hilo.
 Mashabiki wakishangilia ndugu zao walipokuwa wakipita jukwaani
 Rashinda Wanjara (katikati) akiwa na wadau wengine wa Urembo mjini Morogoro.
Jopo la majaji likishauriana jambo wakati wa kutoa maamuzi yao.
Posted by MROKI On Sunday, September 02, 2012 1 comment

1 comment:

  1. Asante Kaka,

    Nakuaminia Mkubwa Mwenzangu. Haya ndio mambo tunayataka haya.
    Saafi sana

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo