Nafasi Ya Matangazo

October 25, 2025

Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii ambaye ni Mkurugenzi Mkuu Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Bw. Bernard Marcelline akifungua rasmi mkutano mkuu wa tano (5) wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha MNRT SACCOS LTD uliofanyika katika ukumbi wa TANAPA leo Oktoba 25,2025 jijini Dodoma. Kushoto ni Mwenyekiti wa MNRT SACCOS LTD, Bw. Wilfred Msemo na kulia ni Afisa Ushirika Jiji la Dodoma, Fred Raymond.
Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii ambaye ni Mkurugenzi Mkuu Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Bw. Bernard Marcelline akifungua rasmi mkutano mkuu wa tano (5) wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha MNRT SACCOS LTD katika ukumbi wa TANAPA leo Oktoba 25,2025 jijini Dodoma.
Baadhi ya wanachama wa MNRT SACCOS LTD katika hafla ya ufunguzi wa mkutano mkuu wa tano (5) wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha MNRT SACCOS LTD kwenye ukumbi wa TANAPA leo Oktoba 25,2025 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa MNRT SACCOS LTD, Bw. Wilfred Msemo akitoa neno la utangulizi katika hafla ya ufunguzi wa mkutano mkuu wa tano (5) wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha MNRT SACCOS LTD kwenye ukumbi wa TANAPA leo Oktoba 25,2025 jijini Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii ambaye ni Mkurugenzi Mkuu Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Bw. Bernard Marcelline (wa tano kutoka kushoto) katika picha ya Pamoja na viongozi na wanachama wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha MNRT SACCOS LTD MNRT mara baada ya kufungua mkutano uliofanyika katika ukumbi wa TANAPA leo Oktoba 25,2025 jijini Dodoma.
 ******************
Na Mwandishi Wetu- Dodoma
Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha MNRT SACCOS LTD kilicho chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kimefanikiwa kutoa mikopo kwa wanachama wake zaidi ya bilioni 1.2 kwa mwaka ili kuwawezesha kujikwamua kiuchumi.
 
Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii ambaye ni Mkurugenzi Mkuu Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Bw. Bernard Marcelline katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa tano (5) wa chama cha MNRT SACCOS LTD uliofanyika katika ukumbi wa TANAPA leo Oktoba 25,2025 jijini Dodoma.
 
Bw. Marcelline amesema kuwa chama hicho chenye wanachama zaidi ya 700 kimewezesha kuongeza tija na ufanisi katika utendaji kazi kwa kufanya watumishi kuwa watulivu katika maeneo ya kazi kutokana na uhakika wa kipato.
 
“Kutoa mikopo ya zaidi ya bilioni 1.2 kwa mwaka maana yake ni fedha zimeingia kwa wanachama na zimekwenda kufanya shughuli za kiuchumi za maendeleo katika sehemu wanazoishi” amesema Bw. Marcelline.
 
“Nawahimiza watumishi wengine ambao hawajajiunga na saccos wajiunge na sacos hii kwa sababu inakua kwa haraka sana” amesisitiza Bw. Marcelline huku akiwahimiza waliokopa kutumia mikopo hiyo kwa malengo waliyojiwekea na pia kurejesha mikopo hiyo kwa wakati ili kuwajengea uaminifu.
 
Naye, Mwenyekiti wa MNRT SACCOS LTD, Bw. Wilfred Msemo amesema kuwa Saccoss hiyo imefanikiwa kutoa gawio la shilingi milioni 76 kwa wanachama wake, kuchangia katika kuhudumia jamii yenye mahitaji mbalimbali pamoja na kuingiza wanachama wapya 138.
Posted by MROKI On Saturday, October 25, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo