Nafasi Ya Matangazo

January 27, 2025






Na Mwandishi weu, Dar es salaam
Naibu katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN) *Mh. Amina J. Mohamed* ameipongeza serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa mkakati wa kufanya utafiti wa kina wa kijiolojia na utafutaji madini nchini.

Naibu Katibu Mkuu Amina Mohamed ameyasema hayo leo wakati wa mkutano wa pembeni wa Mkutano wa Nishati alipokutana na Waziri wa Madini *Mh. Anthony Mavunde*.

“Naipongeza Tanzania chini ya uongozi wa Mh. Rais Samia ambao umekuja na ubunifu mkubwa katika maeneo mbalimbali.

Mpango wa kufanya utafiti wa kina kupitia Vision2030 ni mpango ambao tunauunga mkono kwa kuwa una lengo la kubaini madini ambayo mnayo na hivyo kujiapanga vyema juu ya uvunaji wa madini hayo.

Dunia hivi sasa ina mahitaji makubwa ya madini mkakati,Tanzania imebarikiwa kuwa na madini hayo kwa uwingi hivyo suala la uongezaji thamani,utunzaji wa mazingira na kulinda jamii zinazoishi katika maeneo ya uchimbaji wa madini ni vyema yakazingatiwa wakati wa uandaaji wa mkakati maalum wa uvunaji wa madini ya kimkakati.

Umoja wa Mataifa kupitia programu zake mbalimbali za utunzaji wa mazingira ipo tayari kuunga mkono jitihada hii kubwa ya serikali ya Tanzania“Alisema Mh. Amina Mohamed

Akizungumza katika mkutano huo,Waziri wa Madini *Mh. Anthony Mavunde* amesema kipaumbele cha sekta ya Madini kwa hivi sasa ni kufanya utafati wa kina ili kuiwezesha nchi kupata taarifa za kiwango na ubora wa madini iliyonayo.

Aliongeza kwamba,Utafiti wa kina utaleta matokeo chanya kwenye maeneo ya kijamii na kiuchumi na hivyo kusaidia kuchochea maendeleo ya Tanzania,kwakuwa pamoja na mafanikio yote ya kwenye sekta ya madini eneo ambalo limefanyiwa utafiti ni asilimia 16% ya eneo la nchi nzima.
Posted by MROKI On Monday, January 27, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo