Nafasi Ya Matangazo

September 25, 2024





🔴Yaahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imekuwa inafanya kazi na benki ya Citibank ya Marekani kwa zaidi ya miaka 35 na imekuwa ikipokea ushauri wa mambo ya kifedha kupitia Benki Kuu ya Tanznaia (BoT).
 
Amesema hayo jana (Jumanne, Septemba 24, 2024) mara baada ya kukutana na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo, Bw. John Dugan, kwenye makao makuu ya benki hiyo, jijini New York, Marekani.
 
“Serikali ya Tanzania inaishukuru sana Benki ya Citibank kwa kuwa imeshiriki katika ujenzi wa uchumi ikiwemo na upatikanaji wa fedha za mikopo, kuishauri Serikali katik amasuala ya fedha na kufadhili miradi mikubwa inayoendelea kujengwa nchini,” alisema.
 
“Benki hii imekuwa ikikopesha makampuni yanayojenga reli yetu ya SGR na ili kuhakikisha wanachangia ujenzi wa uchumi wa Tanzania, na wao pia wamechukua lot moja ya ujenzi wa reli hiyo na kufadhili ujenzi wake. Hali kadhalika uendelezaji wa uwanja wa ndege wa Pemba.”
 
Alisema Tanzania ilipokabiliwa na uhaba wa mafuta ya kuendeshea mitambo na magari, benki hiyo ilitumika kuwasaidia wafanyabiashara kupata mafuta kwa bei nafuu,” alisema.
 
Mbali na ushauri wa masuala ya kiuchumi, Waziri Mkuu amesema benki hiyo kwa kushirikiana na taasisi ya kimataifa ya maendeleo ya Marekani, (U.S. International Development Finance Corporation) pia ilitoa mikopo kwa wafanyabiashara wadogo huku ikiwapatia fursa zaidi akina mama na wadada wanaomiliki biashara zao binafsi.
 
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Citibank ya Marekani, Bw. John Dugan amesema wataendelea kushirikiana na Serikali katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo kama walivyofanya katika mika 40 iliyopita.
Posted by MROKI On Wednesday, September 25, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo