Nafasi Ya Matangazo

September 26, 2024

 
Aliyekuwa Makamu Mkuu wa kwanza Taasisi ya Prof. Burton Mwamila akiongea na watumishi na wanafunzi wa taasisi hiyo wakati wa mjadala wa wazi kuhusu malengo ya uanzishwaji wake jijini Arusha.
*********
ALIYEKUWA Makamu Mkuu wa kwanza Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Burton Mwamila amewetaka wahadhiri, wabunifu na watumishi wa taasisi hiyo, kutumia vipawa ili kutimiza malengo mahususi ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo.

Prof. Mwamila ameeleza hayo wakati wa mjadala wa wazi kuhusu namna taasisi hiyo inavyoweza kuwa mchango mkubwa katika kutatua changamoto za jamii na viwanda kupitia Utafiti na Ubunifu.

“Lengo la kuanzishwa kwa taasisi hii , ni pamoja na kutatua changamoto zinazoikabili jamii na viwanda, ili kuleta majawabu ya changamoto hizo” amesema Prof. Mwamila.

Naye Makamu Mkuu wa taasisi hiyo, Prof. Maulilio Kipanyula ameeleza kuwa, tangu kuanzishwa kwake imefanikiwa kuzalisha wataalamu zaidi ya 215 katika eneo la Sayansi, teknolojia na ubunifu ambao wengi wao wanapatikana katika vyuo na taasisi mbalimbali nchini.

Ameongeza kuwa, baadhi ya bunifu zilizozalishwa ni pamoja na chujio la maji machafu na lenye uwezo wa kuondoa madini ya floride kwenye maji NANOFILTER, Uji tayari kwa ajili ya watoto, wagonjwa na wazee, mtambo wa kuzalisha biogas na jiko lake.

Kwa upande wake Prof. Lilian Pasape Amidi wa Shule Kuu ya Mafunzo ya Biashara na Sayansi za Jamii ametoa shukrani kwa Prof. Mwamila kutembelea taasisi hiyo kwa kueleza kuwa, ametoa mwanga kwa waliohudhuria mjadala huo wa wazi hususani namna ambavyo taasisi hiyo inavyoweza kuwa na mchango mkubwa katika kutafuta majawabu ya changamoto za jamii na viwanda, ushirikiano kati ya taasisi na mashirika ya umma na binafsi ili kukuza uchumi wa taasisi pamoja na kuzingatia kutoa huduma bora kwa wateja.

Aliyekuwa Makamu Mkuu wa kwanza Taasisi ya Prof. Burton Mwamila akiongea na watumishi na wanafunzi wa taasisi hiyo wakati wa mjadala wa wazi kuhusu malengo ya uanzishwaji wake jijini Arusha.

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Maulilio Kipanyula Kipanyula akieleza mafanikio ya taasisi hiyo katika eneo la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu wakati wa majadala wa wazi jijini Arusha.

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Maulilio Kipanyula (Kulia) akimkabidhi Prof. Burton Mwamila aliyekuwa Makamu Mkuu wa kwanza wa taasisi hiyo (Kushoto) Tuzo kwa kutambua mchango wake katika tafiti na ubunifi katika taasisi hiyo.

Alikuwa Makamu Mkuu wa kwanza wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof Burton Mwamila (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya taasisi hiyo.


Posted by MROKI On Thursday, September 26, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo