Nafasi Ya Matangazo

September 11, 2024




Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam
Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde ametangaza kukamatwa kwa madini ya dhahabu kilo 15.78 bandarini yalipokuwa yakitoroshwa.

Waziri Mavunde amesema hayo leo tarehe 11 Septemba, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na vyombo vya habari.

"Nchi yetu inazo sekta kadhaa za uzalishaji ambazo mapato yake ndiyo msingi wa maendeleo ya  uchumi wetu ikiwemo sekta ya madini. Sasa basi, tunapokuwa na watu wachache ambao wanajihusisha na vitendo vya utoroshaji wa madini kuikosesha Serikali mapato hatuwezi kuwavumilia" amesema Mavunde

"Kilo hizo 15.78 kwa bei ya leo zina thamani ya takribani *bilioni 3.4* fedha ambazo kwa sasa zote watoroshaji hawa wanakwenda kuzipoteza. Serikali tunakwenda kufuta leseni zao wakitiwa hatiani na mahakama na kuwaweka kwenye orodha ambayo hawataruhusiwa kumiliki Leseni ya kufanya biashara yeyote katika mnyororo wa thamani wa madini Nchini Tanzania", amebainisha Mavunde.

Akielezea kuhusu  uchunguzi unaoendelea, Waziri Mavunde ameeleza kuwa,  watuhumiwa wamesema madini hayo ya dhahabu walikuwa wanasafirisha kutoka bandari ya Dar es Salaam kuelekea Visiwani vya  Zanzibar.

Mavunde amefafanua kuwa, kwasasa Uchunguzi na Mahojiano kwa  watuhumiwa unaendelea na pindi kazi hii ikikamilika tutawapandisha mahakamani ili kujibu mashtaka husika.

Sambamba na hapo, Waziri Mavunde amepongeza kazi nzuri  inayofanywa na Kikosi kazi cha kuzuia utoroshaji wa madini kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama 

Waziri Mavunde ametoa  rai kwa wafanyabiashara nchini kuacha tabia ya utoroshaji madini kwasababu  inarudisha nyuma juhudi za Serikali za  kukuza uchumi wa Nchi yetu.
Posted by MROKI On Wednesday, September 11, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo