Nafasi Ya Matangazo

August 01, 2024

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipewa maelezo na Mkurugenzi wa Bodi ya Kahawa Primus Kimario Mradi wa kuongeza unywaji Wa kahawa nchini kwa kutumia  migahawa Inayotembea ambayo inasimamiwa na mradi wa Jenga Kesho Iliyobora (BBT), alipofungua maonesho ya Kimataifa ya Wakulima ya Nanenane ambayo kitaifa yanafanyika Jijini Dodoma, kwenye viwanja vya Nanenane Nzuguni, Agosti 01, 2024. kushoto ni  Waziri wa Kilimo Hussein Bashe
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipewa maelezo na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kuhusu power tiller za  Kampuni ya Uagizaji wa Matreka ya Agricom wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Kimataifa ya Wakulima ya Nanenane ambayo kitaifa yanafanyika Jijini Dodoma, kwenye viwanja vya Nanenane Nzuguni, Agosti 01, 2024. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipewa maelezo na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kuhusu power tiller za  Kampuni ya Uagizaji wa Matreka ya Agricom wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Kimataifa ya Wakulima ya Nanenane ambayo kitaifa yanafanyika Jijini Dodoma, kwenye viwanja vya Nanenane Nzuguni, Agosti 01, 2024. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia Kahawa iliyotengenezwa na kijana Abdul Issa (kulia) kupitia Mradi wa kuongeza unywaji wa kahawa nchini kwa kutumia migahawa Inayotembea ambayo inasimamiwa na mradi wa Jenga Kesho Iliyobora (BBT) wakati alipofungua maonesho ya Kimataifa ya Wakulima ya Nanenane ambayo kitaifa yanafanyika Jijini Dodoma, kwenye viwanja vya Nanenane Nzuguni, Agosti 01, 2024. Katikati ni Mkurugenzi wa Bodi ya Kahawa Primus Kimario
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia kichwa cha alizeti wakati alipofungua maonesho ya Kimataifa ya Wakulima ya Nanenane ambayo kitaifa yanafanyika Jijini Dodoma, kwenye viwanja vya Nanenane Nzuguni, Agosti 01, 2024. Kulia ni Waziri wa Kilimo Hussein Bashe
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua Mradi wa kuongeza unywaji wa kahawa nchini kwa kutumia migahawa Inayotembea ambayo inasimamiwa na mradi wa Jenga Kesho Iliyobora (BBT) wakati alipofungua maonesho ya Kimataifa ya Wakulima ya Nanenane ambayo kitaifa yanafanyika Jijini Dodoma, kwenye viwanja vya Nanenane Nzuguni, Agosti 01, 2024. Katikati ni Mkurugenzi wa Bodi ya Kahawa Primus Kimario 
Baadhi ya washiriki wa maonesho ya Kimataifa ya Wakulima ya Nanenane wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati alipofungua maonesho hayo ambayo kitaifa yanafanyika Jijini Dodoma, kwenye viwanja vya Nanenane Nzuguni, Agosti 01, 2024.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua maonesho ya Kimataifa ya Wakulima ya Nanenane ambayo kitaifa yanafanyika Jijini Dodoma, kwenye viwanja vya Nanenane Nzuguni, Agosti 01, 2024.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua maonesho ya Kimataifa ya Wakulima ya Nanenane ambayo kitaifa yanafanyika Jijini Dodoma, kwenye viwanja vya Nanenane Nzuguni, Agosti 01, 2024.
********************
TANZANIA imepata dola za Marekani Bilioni 2.32 kwa kuuza tani milioni 1.57 za mazao ya matunda na jamii ya kunde huko China, India, Marekani, Pakistan na Brazil.

Hayo yamesemwa leo (Alhamisi, Agosti Mosi, 2024) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akizungumza na viongozi na wananchi mbalimbali waliohudhuria ufunguzi wa Maonesho ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Sherehe za Nanenane ya Mwaka 2024 katika viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma.

“Kwa upande wa kilimo, hadi kufikia Juni, 2024 Serikali imewezesha upatikanaji wa masoko katika nchi za China, India, Marekani, Pakistan na Brazil ambapo tani milioni 1.574 za mazao ya matunda na jamii ya kunde zenye thamani ya dola za Marekani bilioni 2.329 zimeuzwa katika nchi hizo,” amesema.

Waziri Mkuu amesema Serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko imeingia makubaliano ya kuuza tani milioni 1.25 za mahindi. “Kati ya hizo, tani 650,000 zitauzwa Zambia; tani 500,000 zitauzwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na tani 100,000 kwa Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa.”

Aidha, Waziri Mkuu amesema Serikali imewezesha upatikanaji wa soko la vanilla, pilipili manga, karafuu, nanasi, kakao, viazi mviringo, tumbaku na ndizi katika nchi za China, Marekani, Pakistani, Afrika Kusini na India ambayo yanatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni.

“Kwa upande wa wafugaji, hadi Aprili, 2024 jumla ya tani 13,745 za nyama zenye thamani ya dola za Marekani milioni 56 zimeuzwa katika nchi za Bahrain, Comoro, Hong Kong, Jordan, Kenya, Kuwait, Oman, Qatar, Rwanda, Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu na Vietnam. Pia vipande 1,542,916 vya ngozi vyenye thamani ya shilingi bilioni saba vimeuzwa katika nchi za Nigeria, Togo, Kenya, Ethiopia na Pakistan.”  

Kwenye sekta ya uvuvi, Waziri Mkuu amesema hadi kufikia Aprili, 2024, tani 41,271 za mazao ya uvuvi na samaki hai wa mapambo 134,572, wenye thamani ya shilingi bilioni 515.78, waliuzwa katika nchi za Umoja wa Nchi za Ulaya, Canada, Marekani, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, China, Zambia, Uganda na Malawi. 

Akielezea jitihada ambazo zimechukuliwa na Serikali kuendeleza sekta za kilimo, mifugo na uvuvi, Waziri Mkuu amesema sambamba na utashi na maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Serikali imeendelea kuongeza ajira kwa vijana na wanawake kupitia programu ya Jenga Kesho Iliyobora.

“Kupitia programu hiyo, vijana 686 wanaendelea na kilimo biashara katika mashamba ya pamoja na tayari wameanza uzalishaji. Kwa upande wa mifugo, vijana 161 wanaendelea na programu ya unenepeshaji wa ng’ombe katika vitalu vya Ranchi za Taifa (NARCO). Sekta ya uvuvi nayo haikuachwa nyuma tayari vijana 200 wamehitimu mafunzo na vijana 300 wanaendelea na mafunzo ya ukuzaji wa viumbemaji.” 

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na hadhira hiyo, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alisema wizara yake imeanza kutekeleza maagizo ya Rais Samia ya kujenga miundombinu ya kudumu kwenye viwanja vya kanda yanakofanyika maonesho ya NaneNane ili kuwezesha maeneo hayo kufanya kazi mwaka mzima.

Alisema uwanja wa Nzuguni ambao unahudumia mikoa ya Dodoma na Singida, utajengwa kwa awamu tatu hadi kukamilika kwake na utagharimu sh. bilioni 40. “Tumeanza kujenga uzio, kutakuwa na maeneo shughuli za uzalishaji kwa mwaka mzima, kutakuwa na kumbi za mikutano, incubation centers kwa ajili ya vijana wanaofanya shughuli za teknolojia.” 

Amevitaja viwanja vingine vitakavyoboreshwa kuwa ni vya Johh Mwakangale (Mbeya), Julius Nyerere (Morogoro) Themi (Arusha) na Ngongo (Lindi). Alisema mwakani, vitaanza kujengwa viwanja vya kanda ya Magharibi na Kanda ya Ziwa.

Amesema kwenye kilele cha maadhimisho hayo Agosti 8, mwaka huu, Rais Dkt. Samia anatarajiwa kuzindua kiwanda cha kuunganisha matrekta kinachojengwa hapohapo Nzunguni na vifaa kwa ajili ya wakulima. Atazindua matrekta 500 na powertiller 800 za kwanza.

Amesema lengo ni kuzalisha matrekta 10,000 ifikapo mwaka 2030 ili wakulima wadogo waweze kukodi. “Mkulima hana haja ya kununua trekta kwa shilingi milioni 60, anahitaji shamba lake lilimwe kwa trekta, lipigwe harrow, lipandwe kwa planter, apate boom sprayer. Serikali inawekeza fedha kwenye eneo hilo,” amesema.

Naye, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Alexander Mnyeti alisema kwa muda wa siku nane za maonesho hayo, washiriki watashuhudia mashindano ya mifugo ili kila mfugaji aone kuwa matumizi ya teknolojia ya mifugo yanawezekana kufanyika katika maeneo yao.


Posted by MROKI On Thursday, August 01, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo