Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi,Daniel Sillo akipokea salamu za heshima kutoka kwa Uongozi wa Juu wa
Jeshi la Magereza baada ya kuwasili Makao Makuu ya jeshi hilo yaliyopo Msalato
katika ziara ya kujitambulisha na kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na
jeshi hilo,ziara hiyo imefanyika leo jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi,Daniel Sillo akipokea salamu za heshima baada ya kuwasili Makao Makuu
ya Jeshi la Magereza yaliyopo Msalato katika ziara ya kujitambulisha na kukagua
shughuli mbalimbali zinazofanywa na jeshi hilo,ziara hiyo imefanyika leo jijini
Dodoma.![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhrjDZvg8ea6Y9Twv1k_QuObGkmYDF_c7lsHHI1pV0TnK2G5JYLJluewfWhniTxWjWtDpOJfqiz_tdAqTwJGqViRLULKb0ot1rRLvVDt_DQw-SxbpY2Q9AwBcI_DtuFvidyEQ6Abk9xVvCD3xJ4FWyMBCWEMsJ5Z1L5e6N4URfXxFp0k8sOZlFveL6pBHQ/w640-h426/PIX%200.JPG)
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi,Daniel Sillo(wanne kulia) akiwa
katika picha ya pamoja na uongozi wa juu wa Jeshi la Magereza katika Makao
Makuu ya jeshi hilo yaliyopo Msalato katika ziara hiyo ya kujitambulisha na
kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na jeshi hilo,ziara hiyo imefanyika
leo jijini Dodoma.![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjXhtRz6Nvoq6Wk1A_nrvDt5ANxPH1azzFnIoGKIpJa1qW20dagKHsHpoYphLDHU9XRVhXYl6PAk9LlqL1nLfx44z0cwWCjRWL1574lGSkmEo16mCRrYcVnMxPykpAKAVsa_5wJYC8m07kPTVzR3_mACmTi3FUok8nwl1n_GbznNA2qGovBoAqUCId267c/w640-h426/PIX%203.JPG)
Naibu Kamishna wa Jeshi la
Magereza, Jeremia Katungu wakati akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi,Daniel Sillo wakati wa mkutano uliohusisha Uongozi wa juu wa
jeshi hilo wakati wa ziara ya Naibu Waziri ya kujitambulisha na kukagua
shughuli mbalimbali zinazofanywa na jeshi hilo.Ziara hiyo imefanyika leo jijini
Dodoma.![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg2tcE6YydewOlvl_Q-68zqiIorTDQTPtHFLrcsBq6MkE14aV_SPZf2WvN6PlayhHVm-86DVYIvtSHJUSr-XHvMPYp6iNj2A3hw123ih1hLOeo_YmXxQpzRLsedNvN0YKnOFwxFneLaKDzTiZfBeBLeaKeOKE0fmi-dsFar5D3kjrrATNVlA9bYcQk4fGc/w640-h426/PIX%204.JPG)
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi,Daniel Sillo(wanne kulia) akiwa
katika picha ya pamoja na uongozi wa juu wa Jeshi la Magereza katika Makao
Makuu ya jeshi hilo yaliyopo Msalato katika ziara hiyo ya kujitambulisha na
kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na jeshi hilo,ziara hiyo imefanyika
leo jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
****************
Na Mwandishi Wetu,Dodoma
Serikali imeanza Ufungaji wa Kamera maalumu(CCTV) katika
maeneo mbalimbali yanayozunguka magereza lengo ikiwa ni Uboreshaji wa Huduma za
ulinzi na usalama pamoja na kwenda na dhana
nzima ya sayansi na teknolojia katika utoaji na ufuatiliaji wa huduma kwa wadau
mbalimbali wanaoshilikiana na Jeshi la Magereza ikiwemo Jeshi la Polisi na
Mahakama.
Hayo yamesemwa leo na Naibu
Kamishna wa Jeshi la Magereza, Jeremia Katungu wakati akizungumza mbele ya Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Daniel Sillo wakati wa mkutano uliohusisha
Uongozi wa juu wa jeshi hilo,Maafisa,Askari na watumishi raia huku akitaja baadhi ya mikoa ambapo kamera
hizo zimefungwa.
‘Tunaishukuru Serikali ya
Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri
Jeshi Mkuu, Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuliwezesha jeshi katika maeneo
mbalimbali ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake, baadhi ya
maeneo hayo ni ununuzi wa vifaa vya ulinzi na usalama katika maeneo
yanayozunguka magereza kwa nje ambapo
kwa sasa zoezi la usimikaji wa vifaa hivyo kwa sasa unaendelea katika maeneo ya
magereza ya Maweni, Karanga, Moshi, Lwanda na Tabora’.alisema
Ameyataja maeneo mengine
yaliyoboreshwa na serikali ya awamu ya sita kuwa ni vyombo vya
usafiri,ajira,upandishwaji vyeo kwa askari na maafisa ambapo hadi sasa jumla ya ajira 662 ziko katika mchakato wa
usaili huku upandishwaji vyeo mpaka sasa askari na maafisa 4111 wamepandishwa
vyeo.
Akizungumza katika kikao
hicho, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Daniel Sillo amewataka Askari wa
Jeshi la Magereza kuwa ni nidhamu katika utendaji wao wa kazi ili kujiepusha na
tuhuma mbalimbali ambazo zitalichafua jeshi huku akimpongeza Rais Daktari Samia
Suluhu Hassani kwa msaada anaotoa kwa vyombo vya ulinzi na Usalama likiwemo
Jeshi la Magereza.
‘Sifa kubwa ya askari ni
nidhamu,nidhamu hiyo inapaswa kuanzia ndani ya jeshi mpaka nje,nawaomba
muendelee kuboresha nidhamu kazini ili kuboresha mahusiano yenu pamoja na viongozi
wenu jueni mheshimiwa Rais anawategemea sana katika utoaji wa huduma na
maelekezo yake ni kuwa Tume ya Haki Jinai ilishatoa mapendekezo sasa yafanyiwe
kazi ili kuondoa baadhi ya changamoto ikiwemo msongamano wa wafungwa
magerezani’ alisema Naibu Waziri
Naibu Waziri Daniel Sillo
ameaza ziara rasmi katika vyombo vya ulinzi vilivyopo ndani ya wizara baada ya
muda mfupi kuteuliwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuhudumu katika nafasi
hiyo.
0 comments:
Post a Comment