Nafasi Ya Matangazo

April 29, 2024

Kuna taarifa inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikisema "Ndugu zangu mimi ni Aisha Madoga tumezingilwa na watu wenye Bunduki hapa UDOM......"
 
Taarifa sahihi ni kwamba walinzi wanaolinda eneo la Chuo hicho waliwazuia watu walioingia usiku chuoni hapo wasiendelee kuzunguka eneo la chuo huku  wakiwahamasisha Wanafunzi wawaunge mkono na washiriki katika maandamano wanayoyaandaa Jijini Dodoma.
 
Aidha, Mkuu wa Kituo cha Polisi cha eneo hilo aliwasiliana na mmoja wa kiongozi wa watu hao na kilichoonekana ni kuzuiwa kuendelea kuzunguka ndani ya chuo isivyo halali nyakati za usiku. 

Hivyo waliowazuia ni askari kwa kuzingatia sheria kwa sababu walichokuwa wanafanya chuoni hapo hawakuwa na uhalali wa kufanya hivyo tena nyakati za usiku.
 
Jeshi la Polisi lingependa kuwaonya watu wa aina hii wanaofanya vitendo vya kihalifu kama hivyo na kama haitoshi wanatunga ujumbe wa uwongo na kuusambaza kwenye mitandao kwa lengo la kuwadanganya na kupata huruma ya wananchi ili kuhalalisha vitendo ambavyo havina Baraka za kisheria. 

Watambue kuwa  hatua za kisheria lazima zitachukuliwa dhidi yao endapo wataendelea na tabia hizo.
Posted by MROKI On Monday, April 29, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo