Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kitengo cha huduma za kisheria kwa kushiriki na kitengo cha Ofisi ya Kamshina wa ardhi wa Jiji la Dodoma wanawakaribisha wananchi wote wa Mkoa wa Dodoma kupita katika Banda la Mkoa wa Dodoma lililopo katika viwanja vya Nyerere square' ili kujipatia huduma mbalimbali za msaada wa kisheria kutoka kwa mwanasheria wa Mkoa huo Bw. Jofrey Pima.
Maonyesho hayo yanafanyika ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Sheria iliyoanza tangu januari 24 na inatarajiwa kutamatika kesho januari 30/2024.
Aidha,Huduma zinazotolewa na banda hilo ni pamoja na utoaji wa namba za miamala kwa ajili ya malipo ya hati (control number),kupokea na kutatua changamoto mbalimbali za wateja zinazohusu ardhi,kusajili usajili wa hati na nyaraka za ardhi sambamba na kuelimisha jamii matumizi sahihi ya ardhi.
0 comments:
Post a Comment