*Hizi hapa dondoo 15 muhimu za kuzingatia dhidi ya propaganda hasi kwa bandari ya DSM
1.Magati yote 12 pamoja na maeneo ya kuhudumia shehena za mafuta yanahudumia meli hadi kufikia muda huu wa leo tarehe 28 Januari 2024, tofauti na wapotoshaji wanaoposha kwa makusudi kuwa ni magati mawili (2) tu ndio yanayofanya kazi kati ya magati 12 yaliyopo.
2.Taarifa zinaonesha ukweli halisi watu wakichapa kazi katika magati yote 12 na kuongeza ufanisi. Kwa mfano, Gati namba Sifuri (0) ambalo ni mahsusi kwa kushusha shehena ya magari nalo linahudumia meli MV Yangze 32 ya mizigo mchanganyiko.
3. Idadi na wingi wa meli bandarini unabadilika ukiona leo foleni meli 20 na keshokutwa ukaona meli 20 haina maana ni zilezile maana yake kuna meli zimehudumiwa na nyingine zimekuja kutaka kuhudumiwa.
4. Ni sawa na shuleni mtu anaweza kuhoji mbona kila mwaka shule zinakuwa na wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne. Maana yake ni kuwa kadri wengine wanavyomaliza shule ndivyo wengine wanaanza shule, wa kidato cha nne akimaliza wa kidato cha tatu anapanda cha nne, wa cha pili anapanda cha tatu, wa cha kwanza anapanda cha pili na aliyemaliza shule ya msingi anapanda cha kwanza ni mzunguko. Ndivyo mzunguko wa meli unavyokuwa
5. Mara kadhaa TPA wametufafanulia kuwa meli kuongezeka ni neema sio laana. Tumshukuru Mungu kila meli zinapoongezeka maana yake ajira zinaongezeka, mapato yanaongezeka, makusanyo yanaongezeka na mzunguko unaongezeka.
6. Ni rahisi kusema kuwa meli zinakimbia bandari ya Dar zinakimbilia Mombasa lakini kiuhalisia huu ni uongo na hautekelezeki.
7. Tabia za kibiashara za bandari ya Dar zinaifanya iwe ya kipekee kwa wenye meli kwa kuwa wana uhakika wa kupata mzigo wa kurudi unaotokana na exportation ya nchi jirani hasa madini tofauti na Mombasa ambayo haina mzigo wa kurudi.
8. Haiingii akilini pia kusema mteja wa mzigo kutoka Lusaka Zambia akashushe mzigo wake Mombasa kisha autembeze kutoka Kenya-Tanzania-Zambia wakati anao uwezo wa kutumia Bandari ya Dar moja kwa moja.
9.Kuna tofauti kubwa sana kati ya ongezeko la meli bandarini na ufanisi kupungua (Ongezeko la meli ni kielelezo cha kukua kwa biashara, hata wenye mashule wanapenda wanafunzi waongezeke). Ni muhimu kufahamu kuwa, ufanisi wa Bandari ya Dar ni moja kati ya vivutio vya ujio wa meli nyingi. Kupungua kwa ufanisi kungepimwa na kushuka kwa mapato, kuongezeka kwa muda wa kupakua na kupakia meli. Lakini badala yake mapato yamepanda na muda wa kupakua na kupakia meli umezidi kupungua-Wanastahili pongezi kwenye hili.
10. Ni makosa makubwa sana kuilinginanisha bandari ya Dar na ya Mombasa kiufanisi, uwekezaji na kimuundo
11. Kimuundo Bandari ya Dar ina jumla ya magati 12 na maeneo makuu mawili ya kuhudumia shehena ya mafuta. Bandari ya Mombasa ina magati 22 tofauti yake bandari ya Dar ni nusu ya Bandari ya Mombasa kiukubwa.
12. Kiufanisi bandari ya Dar inapaswa kuhudumia mzigo nusu ya bandari ya Mombasa lakini mwaka Jana Mombasa yenye magati 22 wamehudumia tani takribani milioni 28 huku Bandari ya DSM yenye magati 12 ikahudumia tani milioni 22. Kihesabu ilipaswa kuzidiwa tani milioni 12.
13. Kiutendaji bandari ya DSM inaikimbiza sana bandari ya Mombasa ukilinganisha miondombinu na vifaa walivyonavyo.
14. Sio kweli kwamba Bandari ya Mombasa haijazidiwa na meli, pamoja na kuwa na magati mara mbili ya bandari ya DSM lakini nayo imekiri kuongezeka kwa meli na kwamba wateja wake wawe na subira katika upakuaji mizigo.
15. Kila tunaposikia matangazo ya mapato ya makusanyo kutoka .mamlaka ya Mapato nchini TRA tufahamu kwamba wastani wa asilimia 40 ya makusanyo hayo yanatokana na ushuru wa forodha unaotokana na bandari ya DSM.
0 comments:
Post a Comment