Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule tarehe 26/09/2023 amefanya ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya kimkakakati iliyopo katika Halmashauri ya jiji la Dodoma katika eneo la Nala na Msalato.
Akizungumza na wadau walioshiriki kwenye ziara hiyo amesema Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa kipaumbele kwenye mambo mengi ikiwemo Elimu hivyo ametoa shime kwa wazazi kuhakikisha watoto waliopangiwa kwenda kidato cha tano na bado hawajaripoti wahakikishe wanafanya hivyo mara moja.
Amesema Swala la Elimu ni jambo la muhimu sana kwa kila mwanafunzi kupata elimu iliyo bora na ndio maana Rais hachoki kuleta miradi.
“Kila mzazi ambaye mtoto wake hajaripoti shule ahakikishe anakuja shule kuripoti kwa mara ya kwanza watoto wote waliofaulu kidato cha tano lazima wachanguliwe na waende shule kwani kuna shule nyingi zimejengwa kwaajili ya wao kupata elimu.
“Kwa dhamira njema kabisa ya Mhe Rais ya kuongeza wataalamu katika nyanja mbalimbali katika nchi yetu ni lazima watoto wetu wapate Elimu na tuhakikishe watoto wanafika shule”Amesema Senyamule.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Msalato Bi. Mwasiti B.Msokola amesema shule ya wasichana ya msalato ilipokea fedha toka serikali kuku kiasi cha shilingi Milioni Mia mbili na sitini tu.
Mi
“Ikiwa fedha kwaajili ya ujenzi wa mabweni 02, kwa lengo la kuwapokea wanafunzi Mia mmoja arobaini na mbili (142) wa kidato cha Tano ujenzi huu unatekelezwa kwa kitumia utaratibu wa force account.
Pia katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule ametembelea eneo ambalo litajengwa hospitali katika maeneo ya Nala na ujenzi wa shule ya sekondari Mpamaha kata ya Miyuji.








0 comments:
Post a Comment