Chemba ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) jana imewahimiza wafanyabiashara na wenye viwanda nchini kuchangamkia
fursa ndani ya Soko Huru la Afrika (African Continental Free Trade Area
(AFCFTA) kwa kuwa sasa TCCIA inatoa vyeti vya uasili ambavyo vinaeleza bidhaa
za Tanzania zinakokwenda na kumpunguzia ushuru mfanyabiashara.
Akizungumza kwenye mafunzo hayo ya siku
moja yaliyoandaliwa na TCCIA, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TCCIA, Bi
Mwanahamisi Hussein, amewahimiza wafanyabiashara na wenye viwanda wa Tanzania
kujinufaisha na fursa zilizomo katika soko huru la Afrika ili Tanzania ipate
fedha ya kigeni na kukuza uchumi wa taifa.
“ Tunatoa mafunzo haya kuhakikisha
wafanyabiashara wa Tanzania wananufaika na fursa kwenye soko huru la aflrika na
kufahamu faida zake. Faida moja wapo ya kutumia siko hilo kuongeza wigo wa masoko ya bidhaa za
Tanzania, kukuza viwanda vyetu na kuongeza ajira,” alieleza Bi Mwanahamisi na
kuongeza kwamba TCCIA ina wajibu wa kuunga mkono juhudi ya serikali ya awamu ya
sita ambayo inatoka kipaumbele kwa shughuli za sekta binafasi.
Alisema kwamba Tanzania ni kati ya nchi ambazo zimeingia
katika mikataba mizuri ya masoko mbalimbali duniani ikiwemo soko huru la
Afrika, na kufafanua kwamba TCCIA inataendelea kutumia fursa ya mafunzo kama
hayo kuwafikishia taarifa
wafanyabiashara na kuhakikisha wanazalisha bidhaa zennye ushindani katika soko huru la Afrika.
“Tunataka Tanzania ifanye biashara. Hatutaki
Tanzania iwe soko la bidhaa za nchi nyingine tu. Tunataka tupeleke
bidhaa zetu nchi nyingine hasa kwa kutumia siko hili la Afrika, maana tuna
biashara zinazotakiwa nje ya Tanzania,” alieleza Bi Mwanahamisi.
Mshiriki wa mafunzo hayo, Bi Maria A. Mtui
amesifu mafunzo kwani yamewawezesha
kupata welewa zaidi juu ya fursa katika soko hilo , na kujua aina ya nyaraka
zinazohusiana biashara katika soko hilo.
Bw. Joshua Zuberi amesema mafunzo hayo
yamewafahamisha kwa uwazi zaidi namna wafanyabiashara wa Tanzania
watakavyotumia fursa za soko hilo na kwamba wataweza kufanya biashara katika
masoko makubwa pasipo kutozwa ushuru.
“Hata wateja wetu watafurahia kufanyabiashara pasipo kutozwa
ushuru. Hili ni jambo zuri katika
kufanya biashara,” alisema.







0 comments:
Post a Comment