Nafasi Ya Matangazo

July 23, 2023

Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete akiwasha mshumaa ambao ni ishara ya Upendo kwa wauguzi.
Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete akishirikiana na wauguzi kugawa zawadi mbalimbali katika wodi ya wazazi.
Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete akiangalia muuguzi akitoka huduma  kwa mama aliyejifungua katika wodi ya wazazi Hospitali ya Msoga Chalinze.
Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete akiwa na viongozi mbalimbali wa Chama cha Wauguzi.
Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete akizungumza na wauguzi na kuwaasa kuwa wazalendo.
Wauguzi wakiwa katika maadhimisho hayo.

Msoga, Chalinze

Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete amewataka wauguzi nchini kuwa wazalendo na kutekeleza majukumu yao kwa weledi kwa kufuata maadili.

Kikwete ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze na ameyasema hayo Julai 22,2023 wakati alipoungana na Wauguzi wa Mkoa wa Pwani kuazimisha siku ya Wauguzi Kimkoa sherehe zilizofanyika Ukumbi wa Halmashauri Chalinze, Mkoa wa Pwani. 

Kikwete alisema huku akiwasisitiza kuwa Serikali ya awamu ya sita inatambua changamoto zinazowakabili wauguzi na kuwaahidi kuwa serikali inaendelea kuzishughulikia ikiwa pamoja na mifumo ya kusaidia Utendaji bora wa kazi.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ya kimkoa ilikua "Wauguzi wetu mstakabali wa Afya zetu"

Sherehe hizo zilitanguliwa kwa wauguzi hao pamoja na Naibu Waziri kutembelea Hospitali ya Wilaya ya Chalinze, Msoga.

Wakiwa Hospitalini hapo, Naibu Waziri akiongozana na Wauguzi wa Mkoa wa Pwani walipata nafasi ya kutembelea wodi ya Wazazi ambapo pamoja na shughuli nyengine waligawa taulo za watoto wachanga, sabuni za kufulia na kuogea kwa wazazi wote waliojifungua watoto.
Posted by MROKI On Sunday, July 23, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo