Nafasi Ya Matangazo

March 09, 2023


Mkurugenzi wa Kampuni ya Weka Jiji Safi (WEJISA Company Ltd),Bi.Nuru  Hassan akizungumza na kupongeza juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira mazuri ya kufanya kazi ikiwemo wafanyakazi Wanawake, jambo ambalo limeongeza uchapakazi Kwa Jinsia hiyo.
Wanawake wakifurahia
Na Mwandishi Wetu,
Kampuni ya Weka Jiji Safi (WEJISA Company Ltd) kupitia kwa Mkurugenzi Mkuu wake Bi.Nuru  Hassan amepongeza juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuweka mazingira mazuri ya kufanya kazi ikiwemo wafanyakazi Wanawake, jambo ambalo limeongeza uchapakazi Kwa Jinsia hiyo.

Nuru amesema hayo kwenye maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani ambayo inafanyika Machi 8 ya Kila mwaka.

"Rais wetu Samia tunamuunga mkono kwa sababu nafasi aliyonayo amesaidia kuongeza mwamko kwa wanawake kufanya kazi na wale ambao walikua hawana kazi na kutafuta shughuli zozote ili waweze kujiondoa kwenye utegemezi," alisema Nuru.

Alisema kuwa, kampuni ya WEJISA  itaendelea kushirikiana na Serikali bega kwa bega na ndo maana leo tumekuja hapa kusheherekea pamoja na kujifunza mengi kwa Wafanyakazi wetu Wanawake" alisema Nuru Seif Hassan.

Aidha, amesema kuwa amepata faraja kujumuika na Wanawake hao kwani wamekuwa chachu ya Maendeleo ya Kampuni hiyo.

Wanawake hao wa WEJISA wanatoka vitengo mbalimbali ikiwemo wanaosafisha maeneo ya Jiji, ikiwemo ufagiaji, ukusanyaji wa taka na usafi wa mazingira.

Lengo la tukio hilo ni kupeana moyo kama Wanawake katika kuamua mambo katika kufanikisha utendaji bora wa kazi.

Kwa upande wake Patricia Kimelemeta Mwandishi Kimara wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Mtoto Mkoa wa Dar es Salaam ambaye alitoa mada ya malezi na makuzi Kwa watoto katika tukio hilo la kusheherekea siku ya Wanawake, ambapo alitoa raia Kwa wazazi kuendelea kutoa elimu kwa watoto wao ikiwemo kujenga ukaribu wa kuwachunguza ilikujua changamoto wanazopatana nazo.

Kwa upande wao baadhi ya Wanawake wafanyakazi wa WEJISA waliishukuru kampuni hiyo kwani imekuwa mkombozi kwao na wamekuwa wakifanya kazi moyo.
"Mie nina familia, nikitoka nyumbani naandaa kabisa chakula kwa wanangu.

Aidha, amewataka Wanawake kuzingatia sheria za Usalama barabarani kwani wamekuwa wakishuhudia matukio mengi, ikiwemo wao kugongwa.'  Alisema Bi. Asha Salum.

Kwa upande wake. Bi. Sharifa Magombeka amesema kuwa, anafanya kazi ya kuzoa taka ilikupata kipato chake halali.

"Mwanamke ni kujitambua, nafanya kazi yangu ya kuzoa taka hii kupata kipato kihalali, tunamshuru Mhe Rais kuendelea kueka mazingira ya ufanyaji kazi, Leo tumejumuika hapa tumepata elimu, lakini pia tumefuraia pamoja" alisema Sharifa.
Posted by MROKI On Thursday, March 09, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo