Nafasi Ya Matangazo

December 06, 2019

Mkuu wa wilaya ya longido Frank Mwaisumbe akifungua kongamano la utalii la wanahabari kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo .


Mkuu wa Mkoa Arusha Mrisho Gambo, amewataka Waandishi wa habari Kanda ya Kaskazini kuongeza kasi ya kutangaza vivutio vya Utalii ili kukuza Uchumi wa nchi.


Gambo ametoa ombi hilo wakati akifungua kongamano la tatu la Utalii la Arusha tourism Festival lilikuwa limendaliwa na waandishi wa habari za Utalii na taasisi ya Arusha media na kushirikisha waandishi kutoka mikoa ya Arusha,Kilimanjaro, Manyara na wanafunzi wa vyuo vya uandishi wa habari.

Katika hotuba ya Mkuu wa Mkoa Arusha (Gambo), iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe, Gambo amesema vyombo vya habari vina fursa nzuri ya kukuza Utalii kwani sasa unachangia asilimia 17 ya pato la taifa na asilimia 25 ya fedha za kigeni.
Amesema kongamano hili lililodhaminiwa na shirika la hifadhi za Taifa(TANAPA) taasisi ya chemchem Association na Friedkin Conservation Fund(FCF) lina manufaa makubwa katika kukuza Utalii.

“Wanahabari mnabeba dhamana kubwa katika kutangaza vivutio vyetu, lakini mnapoandika habari mbaya za sekta hii, mnatoa mwanya kwa washindani wetu kuzisambaza kwa nguvu habari hizo ili tusipate watalii, sasa saidieni serikali kutangaza Utalii" amesema.

Amesema ili mtalii aje nchini ni lazima ajihakikishie usalama wake,mali zake na hivyo kumladhimu kutafuta taarifa za nchi husika atakayoenda.
 “Sasa kama mkiandika kuna maandamano,ghasia na vinginevyo washindani wetu watasambaza taarifa hizo kwa nguvu ili wapate watalii wao na sisi tukose,hivyo vema tushiriki wote kutangaza mema tu ya taifa letu, ili tukuze zaidi sekta hii,”amesema.

Amesema Serikali inapambana kuhakikisha sekta hii inakua na ndio maana imenunua ndege, kwani unapokua na usafiri wa uhakika ni moja ya njia ya kuongeza watalii.

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (APC) Claud Gwandu, amesema ni vema wanahabari nchini, wakabadilika katika uandishi wa habari za sekta ya utalii.
“Ili mtalii aje Tanzania ni lazima tuwe na kitu cha ziada na kitu hicho siyo kingine amani,kwani kama wanyama Simba,Twiga,Tembo,Mbogo na wengine nao wapo nchi jirani, sasa sisi tunawajibu  kutangaza amani tuliyonayo kwa nguvu zetu zote,”amesema.

Mkurugenzi wa Taasisi ya wanahabari Arusha ya Arusha Media, Mussa Juma amesema kongamano hilo linafanyika kila mwaka, ili kuongeza ari kwa wanahabari kutambua umuhimu wa kutangaza vivutio vilivyopo nchini.

“Lakini pia Taasisi hii inalenga kujenga uwezo kwa wanahabari, jinsi ya kupiga vita ujangili na kutumia kalamu zao kuhamasisha utalii wa ndani,”alisema.
Akizungumza kwa kongamano hilo, mwenyekiti wa Kanda ya Pwani, Vitalis Makinda Chama cha mawakala wa Utalii nchini(TATO), amesema wanashirikiana na serikali kukuza Utalii.

"Hivi sasa tunajenga vituo vya polisi wa Utalii lakini pia tunamiradi kadhaa kusaidia Utalii ikowepo kuzuia wanaotega nyumbu" amesema.

Hillal Dafi kutoka chama cha wawindaji wa Kitalii (TAHOA) alitaka vyombo vya habari kusaidia kukuza uwindaji wa kitalii kwani una faida kubwa ikiwepo kupiga vita ujangili.
Mtendaji Mkuu cama cha wapagazi mlima Kilimanjaro (TPO) Loshiye Mollel alisema serikali imesaidia sana wapagazi na sasa changamoto nyingi zimepatiwa ufumbuzi.

Afisa Maendeleo ya Jamii taasisi ya Chemchem Foundation, Walter Pallangyo alisema wamekuwa wakitoa udhamini wa wanafunzi lakini wamechangia miradi zaidi ya sh 100 milioni.

Kwa upande wake Makamu mwenyekiti wa Burunge WMA,Emmanula Oalu alisema WMA zina mchango mkubwa katika uhifadhi ma Utalii nchini.
Posted by MROKI On Friday, December 06, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo