Mlezi wa Kikundi cha Wake wa Viongozi cha New Millenium Women Group, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akisoma hotuba yake wakati kikundi hicho kilipokabidhi majengo ya madarasa manne na vyoo kumi kwa Kituo cha waotot wenye ulemavu cha Buhangija wilayani Shinyanga Novemba 10, 2019. Kushoto ni Mgeni rasmi katika makabidhino hayo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako akizindua madarasa manne ya Kituo cha watoto walemavu cha Buhangija wilayani Shinyanga yaliyojengwa kwa ufadhili wa kikundi cha wake wa viongozi cha New Melleanium Women Group. Wa nne kulia ni Mlezi wa kikundi hicho, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa, Wapili kulia ni Mwenyekiti wa kikundi hicho, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mama Tunu Pinda, kulia ni Mama Hasina Kawawa, wa tano kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko.
Mlezi wa kikundi cha Wake wa Vingozi cha Millenium Women Group, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akisalimiana na watoto wa kituo cha walemavu cha Buhangija wilayani Shinyanga baada ya kikundi hicho kukabidhi majengo ya madarasa manne na vyoo kumi kwa shule hiyo, Novemba 10, 2019. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack.
Mlezi wa kikundi cha wake wa Vingozi cha New Millennium Group, Mke wa Waziri mkuu, Mama Mary Majaliwa akikumbatiana na Mwenyekiti wa Kikundi hicho, Mama Tunu Pinda, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu katika hafla ya kukabidhi majengo ya madarasa manne na vyoo kumi kwa Kituo cha Watoto Walemavu cha Buhangija wilayani Shinyanga yaliyojengwa kwa ufadhili wa kikundi hicho, Novemba 10, 2019.
Mlezi wa Kikundi cha Wake wa Viongozi cha New Millenium Women Group, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa (kulia), Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa kikundi hicho, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu , Mama Tunu Pinda (wa tatu kulia) wakiwapa chakula watoto wa kituo cha Watoto wenye ulemavu cha Buhangija wilayani Shinyanga baada ya kukabidhi majengo ya vyumba vinne vya madarasa na vyoo kumi, Novemba 10, 2019.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa ametoa wito kwa wazazi na walezi watoto wenye mahitaji maalumu kutowaficha na kuwatelekeza na badala yake wawape nafasi ya kupata elimu kwa sababu ni haki yao ya msingi.

Mama Majaliwa ambaye pia ni Mlezi wa Umoja wa Wake wa Viongozi (New Mellenium Women Group), ametoa wito huo leo (Jumapili, Novemba 10, 2019), wakati alipokabidhi majengo ya madarasa manne na matundu ya vyoo kumi kwa Kituo cha Watoto Wenye Ulemavu cha Buhangija mkoani Shinyanga yaliyojengwa na umoja huo.
Mama Majaliwa amesema si vyema kuwatenga au kuwakatia tamaa watoto wenye ulemavu kwani wao pia ni watoto sawa na watoto wengine, hivyo wanastahili kupewa haki zote bila kubaguliwa.
Amesema hatua waliyochukuwa akinamama wa umoja huo inaunga mkono jitihada za serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kuwapatia watoto wa kitanzanai elimu bure na katika mzingira mazuri.
Mgeni rasmi katika makabidhiano hayo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa, Joyce Ndalichako ameupongeza umoja huo kwa shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kuwajali watoto wenye mahitaji maalumu.
Profesa Ndalichako amesema katika kipindi cha mwaka 2019/2020 Serikali imetenga jumla ya sh 3,809,758,460.00 kwa ajili ya kununua na kusambaza vifaa vya kufundishia na kujifunzia pamoja na vifaa visaidizi kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum (wakiwemo Albino), katika shule na vitengo vya elimu maalum.
Waziri huyo ameongeza kuwa pamoja na juhudi hizo za Serikali, bado wanafurahi wanapopata michango kama huo uliotolewa leo. "Wito wangu kwenu tusichoke kuwasaidia hawa watoto wetu. Napenda kuwakumbusha na kusisitiza kwamba Watu wenye Ulemavu wanahitaji msaada mkubwa kutoka kwenu."
"Tuwasaidie na tushirikiane kuwapatia mahitaji yao muhimu ikiwa ni pamoja na elimu, huduma za afya na mazingira mazuri ya kuwawezesha kuishi bila ya matatizo. Serikali kwa upande wake itaendelea kujitahidi kwa uwezo kutoa fursa zinazojali mahitaji yao."
Amesema madarasa pamoja na vyoo alivyokabidhiwa leo kwa niaba ya uongozi wa kituo cha Buhangija na Kikundi cha New Millenium ni tunu kwao na wananchi wa Shinyanga na ni sadaka kwa watoto wa Buhangija, hivyo, ameutaka uongozi wa Mkoa na Uongozi wa Kituo kwa pamoja washirikiane kuyatunza vizuri ili yaweze kutumika kwa muda mrefu.
Akitoa taarifa ya ujenzi huo kwa mgeni rasmi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela amesema fedha zilizotumika kwa ajili ya ujenzi wa madarasa manne ni sh. 65m,884,523/= ambapo kila chumba cha darasa kimejengwa kwa wastani wa sh. 16,471,130.
Amesema ujenzi wa vyumba kumi vya vyoo unaendelea na ukikamilika utagharimu sh.26, 271,922.44 na kwamba vyoo hivyo vitakuwa vya kisasa vikiwa na maji ndani pamoja na masinki ya kunawia ili kukidhi mahitaji ya watoto wenye ulemavu.
0 comments:
Post a Comment