Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (katika) akizungumza na Mkurugenzi wa
Kiwanda cha kuchinjia Punda Fang Hua, Lifang Yu, kulia ni Kaimu
Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Masoko wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Assimwe
Lovince.
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akiangalia zizi la Punda na
Mkurugenzi wa Kiwanda cha kuchinjia Punda Fang Hua, Lifang Yu aliye
kushoto kwake.
Punda kwenye zizi la Kiwanda cha kuchinjia Punda Fang Hua mjini Shinyanga.
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (mwenye miwani) katika picha ya pamoja
na watumishi wa Kiwanda cha kuchinjia Punda Fang Hua. Picha na John
Mapepele.
****************************
Na John Mapepele, Shinyanga
WAZIRI wa
Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amewahakikishia wenye viwanda nchini kuwa
hakuna mali ya mifugo ya Tanzania itakayotoroshwa tena kwenda nje ya
nchi kimagendo kwani Tanzania haiwezi kukubali kugeuzwa kuwa machungio
ya mifugo hiyo.
Waziri Mpina ametoa kauli hiyo jana mjini
Shinyanga baada ya kutembelea Kiwanda cha Fang Hua kinachojishughulisha
na uchinjaji wa Punda ambapo alielezea kuridhishwa kwake na juhudi kubwa
zilizofanywa na mwekezaji huyo kuwezesha kuwepo soko la uhakika la
mifugo hiyo.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha Fang Hua, Lifang Yu
alimweleza Waziri Mpina kwamba kiwanda chake kimeshaingia ubia na
wafugaji wadogo wapatao 27 ili kuongeza uzalishaji ambapo kinatarajia
kuwashilikisha wafugaji wengi zaidi katika mikoa mbalimbali nchini
Waziri
Mpina aliwahakikishia wawekezaji wenye viwanda katika sekta ya mifugo
kuwa malighafi hiyo itakuwepo ya kutosha kwani Serikali ya awamu ya tano
chini ya Dk. John Pombe Magufuli haitakubali tena mifugo hiyo kuendelea
kutoroshwa nje ya nchi na kunufaisha viwanda vya nchi hizo.
Hivyo
Waziri Mpina alisema uwekezaji wa aina hiyo wa kuongeza thamani ya
mazao ya mifugo ni moja ya vipaumbele vya wizara yake kwa sasa ili
kuchochea kwa kasi kufanikisha azma ya Tanzania ya viwanda.
Alisema
kiwanda hicho mbali na kuongeza soko la punda pia kimechangia kuchochea
uchumi wa Mkoa wa Shinyanga pamoja na kutatua changamoto ya ajira
ambapo hadi sasa kimeajiri wafanyakazi 100 hivyo alimhakikishia
mwekezaji huyo kuwa changamoto ya punda wengi kutoroshwa nchini Kenya
haitakuwepo tena.
Alisema kwa sasa kuna viwanda viwili vya
kuchakata nyama ya punda na kuuza nchini China, ambapo wastani wa mauzo
ya nyama hiyo nje ya nchi yalifikia tani 2000 mwaka 216/17
Mpina
aliwahimiza wawekezaji hao kuhakikisha wanawasaidia wafugaji katika
kuongeza uzalishaji, kupambana na maradhi, upatikanaji wa maji na
malisho kwa mifugo.
Aliwataka kuanzisha ranchi ya mifugo na maeneo yakupumzishia mifugo hiyo kabla ya kuchinjwa.
Alisema idadi ya punda waliopo nchini ni 520,000 tu hivyo juhudi za makusudi zinahitajika kuongeza uzalishaji.
Kaimu
Mkurugenzi wa Uzalishaji Mifugo na Masoko wa Wizara ya Mifugo na
Uvuvi, Dkt. Lovince Assimwe aliwataka wafugaji kuongeza soko la
uhakika.
Alipongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kubuni mbinu
za kuwasaidia wafugaji kwa kuwapatia shilingi elfu tano kila mwezi
kwa ajili ya matibabu ya punda.
0 comments:
Post a Comment