Kushoto kwenda Kulia ni Charles Kie,
Mkurugenzi Mtendaji wa, Ecobank Nigeria Ltd; Serigne Dioum, Mtendaji wa MTN’s ,
Hudma za kifedha kwa njia ya mtandao; Ade Ayeyemi, Ofisa Mtendaji Mkuu wa,
Ecobank Transnational Incorporated (ETI), Rob Shuter, Ofisa Mtendaji mkuu wa
MTN na Patrick Akinwuntan, Mtendaji wa
Ecobank Transnational Incorporated (ETI)
Na Mwandishi wetu
KAMPUNI ya simu MTN imeingia ubia na moja ya benki
inayoongoza barani Afrika ya Ecobank Transnational Incorporated (ETI)
kuwezesha wateja wao kufaidika na huduma
za kifedha zinazotolewa na makampuni hayo.
Imeelezwa kuwa MTN ikijivunia idadi kubwa ya wateja
wanaotumia huduma zake mbalimbali; mtandao mkubwa wenye uhakika; bidhaa zenye
ubunifu na huduma zake za kifedha kwa mtandao imeungana na Ecobank kuwezesha wateja
wao kuanzisha kufungua akaunti na kupitisha miamala yao kupitia mtandao wa MTN.
Makampuni hayo mawili maarufu barani Afrika yametiliana
saini mkataba wa makubaliano utakaowezesha kushirikiana katika kubuni na
kuwezesha huduma za kifedha zenye ubora wa kiwango cha juu kati ya benki hiyo
na mtandao wa simu wa MTN.
Miongoni mwa huduma zitakazotolewa ni kuwezesha miamala
mbalimbali kufanyika kwa kutumia simu na akaunti za benki.
Kutumia mitaji iliyopo katika uwekezaji ndani ya Ecobank na MTN kuwezesha miamala ya kimataifa
kufanyika kidigitali.
Aidha makubaliano hayo yatachochea ubunifu wa bidhaa
mbalimbali katika upande wa hifadhi ya fedha kwa njia ya mtandao na ukopeshaji
wake na kutoa nafasi ya malipo kwa njia ya mtandao kwa wateja, wafanyabiashara
na mashirika mbalimbali.
Ade Ayeyemi, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Ecobank anasema: “
Mabadiliko ya kidigitali katika mifumo ya benki na simu kunatengeneza fursa za
namna bora ya kuwezesha kutoa huduma za kifedha. Afrika inalazimika kwenda mbio katika digiti ili
kuwezesha fursa zilizopo zitumike kuwatumikia wateja. MTN na Ecobank leo wamechukua hatua kubwa kuwezesha
fursa hizo” .
Pia alisema kwamba
mkakati wa benk hiyo wa kidigiti kwa muda mrefuj umelenga kuhakikisha
nafuu ya uwezeshaji wa miamala katika soko.
Akizungumzia ushirikiano huo Ofisa Mtendaji Mkuu na Rais,
Rob Shuter alisema: “Ushirikiano kati ya mabenki na watoaji wa huduma za
miamala kwa njia ya simu ni muhimu, hivyo uhusiano wetu wa muda mrefu na Ecobank umelenga kuwezesha huduma za fedha
kuwafikia wananchi wengi na kwa urahisi zaidi. Tumefurahishwa na maafikiano haya kwani yametupeleka hatua
nyingine, kwani ushirikiano wetu utawezesha ubunifu utakaowezesha huduma za
fedha kupenya kila mahali katika bara hili.”
0 comments:
Post a Comment