Nafasi Ya Matangazo

January 30, 2018

Baraza la Mitihani la Taifa (NEC), leo limweka hadharani matoneo ya mitihani ya kidato cha Nnne kwa watahiniwa waliofanya mitihani yao Novemba 2017. 
Posted by MROKI On Tuesday, January 30, 2018 No comments
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Makamu wa Rais (Sera na Uratibu), Profesa Faustine Kamuzora (kulia), na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Khamisi Shaaban, wakisaini hati za makabidhiano ya sh. trioni moja zilizotolewa na Shirika la Global Fund kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kusaidia mapambano ya Ukimwi, TB na Malaria katika hafla iliyofanyika Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam leo. Wengine waliosimama katikati ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na viongozi wengine kutoka Global Fund.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk. Mpoki Ulisubisya, akizungumza katika hafla hiyo.
Balozi wa Ufaransa Nchini Tanzania, Frederic Clavier, akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mnufaika wa Global Fund, Joan akielezea jinsi alivyo nufaika na shirika hilo.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu wanaishi na VVU-Ukimwi, Mwinuka Juastine, akizungumza.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Khamisi Shaaban (kulia), akimkabidhi hati ya makabidhiano Mwakilishi wa Global Fund Tanzania, Linden Morrison.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Makamu wa Rais (Sera na Uratibu), Profesa Faustine Kamuzora, akizungumza.
Taswira ya ukumbi wa mkutano katika uzinduzi huo.

Na Dotto Mwaibale
SHIRIKA la Kimataifa la Global Fund limetoa shilingi trioni moja kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya mapambano ya magonjwa ya ukimwi, malaria na kifua kikuu kwa mwaka 2018-2020. 

Akizungumza katika hafla ya kutiliana saini makabidhiano ya fedha hizo baina ya mfuko huo na serikali Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema fedha hizo ni muhimu sana kwa nchi yetu.

Alisema fedha hizo zitaelekezwa katika kupambana na magonjwa hayo ambapo kwa ugonjwa wa ukimwi zimetolewa sh.bilioni 769, TB sh. bilioni 67 wakati malaria sh.bilioni 320.

Alisema fedha hizo zitatumika kikamilifu kwa lengo lililokusudiwa na zitasimamiwa na Ofisi ya Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wizara ya Afya na Mashirika Yasiyo ya kiserikali.

Alisema katika masuala ya ukimwi zitatumika kwa ajili ya vipimo, dawa za kurefusha maisha na kufubaza virusi kwa wagonjwa wa ukimwi na katika ugonjwa wa malaria fedha hizo zitatumika kwa ajili ya vipimo na matibabu pamoja na kununua vyandarua.

"Kwa upande wa wagonjwa wa TB ni asilimia 40 tu ndio waliofika kwenye vituo vya afya na kuthibitika kuwa na maambukizi na wamepatiwa matibabu lakini tunataka hadi ifikapo mwaka 2020 tunataka asilimia 70 ya watanzania watakaogundulika kuwa na maambukizi wajulikane na wapatiwe matibabu" alisema Ummy.

Ummy aliongeza kuwa kati ya wagonjwa 100 wenye maambukizi ya TB wagonjwa 90 waliothibitika kuwa na maambukizi walitibiwa na kupona kabisa.

Katika hatua nyingine Waziri Ummy amewataka Katibu Mkuu wa Wizara yake, Tamisemi na Ofisi ya Rais kuhakikisha wanazisimamia vizuri fedha hizo ili kupata matokeo mazuri waliyo yakusudia.

Mratibu wa Watu Wanaotumia Dawa za Kulevya Tanzania (TANPUD), Happy Assan alisema mradi huo utawasaidia sana na kuhakikisha hawataathirika ukizingatia kuwa fedha hizo zitawafikia walengwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu wanaishi na VVU-Ukimwi, Mwinuka Juastine alisema mradi Global Fund imewasaidia waathirika 900,000 kwa kuwapa dawa za kupunguza makali ya ukimwi ARV na kufubaza virusi vya ugonjwa huo.
Posted by MROKI On Tuesday, January 30, 2018 No comments
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bathow Mmuni ambaye alikuwa mgeni rasmi akifunga mfunzo ya wajasiliamali yaliyoendeshwa na Sido mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Mkurugenzi wa Sido Dar es Salaam, MacDonald Maganga.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bathow Mmuni akiwa ameshika chaki iliyotengenezwa na wajasiliamali waliokuwa waliopata mafunzo ya Sido-Dar es Salaam. 
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bathow Mmuni akionyeshwa nguo ya batiki iliyotengenezwa na wajasiliamali waliokuwa waliopata mafunzo ya Sido-Dar es Salaam. BOFYA HAPA KUONA ZAIDI.
Posted by MROKI On Tuesday, January 30, 2018 No comments

January 29, 2018

Busi la kampuni Ya Tahmeed lenye namba za usajili T483 BFL limeungua moto katika Kijiji cha Kabuku wilayani Handeni mkoani Tanga. 

Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, SACP Edward Bukombe alisema basi hilo ambalo lilikuwa na abiria 9 tu kutoka Dar es salam liliungua moto kutokana na hitilafu za umeme. 

Alisema Dereva wa bus hilo Bakari Said (34) alihisi halipo vizuri katika mfumo wa engine akasimamisha gari kisha kuwaomba abiria washuke.

Hata hivyo hakukuwa na mtu aliyejeruhiwa kutokana na ajali hiyo. Hii ni mara ya pili kwa basi la kampuni hiyo kupata hitilafu Kwenye mfumo wa injini na kuungua moto.
Posted by MROKI On Monday, January 29, 2018 No comments
MBUNGE wa Jimbo la Chalinze, Mkoani Pwani, Ridhiwani Kikwete amefanya ziara ya kukaguamiradi ya maendeleo Latina jimbo lake la Chalinze na safari hit akita ametembelea kijiji cha Mnhindi .

Akiwa kijijini haps, Ridhiwani aliweza kuangalia maendeleo ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji hicho ambayo ujenzi wake unsends kwa kasi na pindi ikikamilika itahudumia wakazi wanaoishi katika Kijiji hicho na Vitongoji Vyake. 

"Tumeshauriana kujipanga kwa ujenzi wa Kituo cha Afya kwa kuwa kukamilika kwa Bandari kavu ya Kwala kuna  athari kubwa pia kwa maendeleo ya kijiji hicho na hitaji la huduma za Afya kwa watoa huduma katika eneo hilo," alisema Ridhiwani.
 Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete akitembezwa kuangalia maendeleo ya ujenzi wa Zahanati hiyo ya Mnhindi.
 Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mnhindi  kama inavyoonekana ilivyofikia sasa.
Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete akitembezwa kuangalia maendeleo ya ujenzi wa Zahanati hiyo ya Mnhindi.
Wakazi wa Kijiji cha Mnhindi wakiwa Latina montano wa hadhara na Mbunge wao (hayupopichani)
Posted by MROKI On Monday, January 29, 2018 No comments
MUDA mfupi baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla kutaja watu waliovamia maeneo ya hifadhi nchini hasa mkoani Arusha, familia ya Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa imejitokeza hadharani na kuzungumzia sakata hilo la baba yao kutajwa kuwa mimosa wawatu waliovamia maeneo ya hifadhi. 

Fredrick Lowassa ndie msemaji wa familia ambaae amezungumzia sakata hilo kwa masikitiko makubwa juu ya jina la Lowassa kutajwa Latika uvamizi huo.

"Nimesikia taarifa za Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangalla akitaja jina la Lowassa kama mmoja ya watu eti walioshiriki kupora ardhi Arusha. 

Nimesikitishwa sana na matamshi hayo kutoka kwa waziri ambaye kwa mtu mwenye wadhifa wake kutoa kauli zisizo na msingi wowote na kulaghai Umma. 

Nimemfahamu Mhe Kigwangalla kwa miaka mingi, tangu wakati anavurugana na mbunge mwenzake wa Nzega na rafiki yangu Mhe Hussein Bashe kule Nzega.

Kwa maoni na mawazo yangu nimekuwa nikiamini kwamba Kigwangalla atakuwa mtu aliyebadilika na kujifunza kutoka na makosa yake ya nyuma.

Kauli yake ya leo ni ushahidi kwamba bado ana matatizo yale yale ya kukurupuka.

Ni wazi hata baada ya mambo mengi kubadilika na pengine nyakati za kuchafua watu kukoma, ndugu huyu bado anaishi nyakati zile zile.

Ni wazi Kigwangalla anatumia vibaya dhamana aliyopewa na Rais Magufuli , kwa mambo ambayo Wizara ya Ardhi ina Wataalamu na uwezo wa kuchukua hatua stahiki kwenye mgogoro wowote.

Nikiwa kama Msemaji wa Familia ninazo katika kiganja cha mikono yangu taarifa zote za umiliki wowote unaomgusa Lowassa.

Ninaweza kuuhakikishia umma kwamba yote aliyosema Waziri Kigwangalla hayapo, na kama anayo basi sisi tuko tayari afanye lolote lililo chini ya mamlaka yake badala ya kurejea kule tulikopita ambako yeye na wenzake kadhaa walifanya bila mafanikio kuchafua heshima za wote anaowataja bila sababu.
Posted by MROKI On Monday, January 29, 2018 No comments


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akipata maelezo ya eneo la kiwanja chenye hati namba 4091 kilichopo Njiro Jijini Arusha ambacho kimevamiwa na watu mbalimbali na kuanzishwa makazi yenye kaya 82 ndani ya eneo hilo kutoka Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Dk. Fredy Manongi (katikati). Eneo hilo ni mali ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na hati halisi ya eneo hilo ipo kwa jinala Bodi ya Utalii Tanzania. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua eneo la kiwanja chenye hati namba 4091 kilichopo Njiro Jijini Arusha ambacho kimevamiwa na watu mbalimbali na kuanzishwa makazi yenye kaya 82. Eneo hilo ni mali ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na hati halisi ya eneo hilo ipo kwa jinala Bodi ya Utalii Tanzania.
Meneja wa Huduma za Sheria wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Egidius Mweyunge (kulia) akimuongoza Waziri Kigwangalla kukagua eneo hilo.
Dk. Kigwangalla akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukagua eneo hilo.
Posted by MROKI On Monday, January 29, 2018 No comments

January 26, 2018

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Wizara hiyo Mjini Dodoma leo. Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Aloyce Nzuki.
**************
Na Hamza Temba - Dodoma
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla leo Januari 25, 2018 mjini Dodoma ametaja majina ya watuhumiwa wa ujangili ambao wengi wao ni wamiliki na washirika wa Kampuni za uwindaji wa kitalii na kuwapa siku saba wawe wamefika kwa hiari yao wenyewe katika ofisi za Wizara hiyo Mjini Dodoma, Swagaswaga House kwa ajili kutoa maelezo kwanini wasichukuliwe hatua za kisheria ikiwemo kujibu tuhuma hiyo na nyingine nyingi zinazowakabili mbele ya kamati atakayoiunda.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Dk. Kigwangalla ametaja baadhi ya tuhuma hizo ambazo ziko kinyume cha sheria na taratibu za uwindaji wa kitalii kuwa ni uwindaji haramu, uhawilishaji wa umiliki wa vitalu vya uwindaji pasipo kufuata sheria, udanganyifu kwenye kujaza fomu za uangalizi,  rushwa, uhalifu dhidi ya rasilimali za wanyamapori na uhujumu uchumi.

Alitaja tuhuma zingine kuwa ni ukiukwaji wa kanuni za uwindaji (kupiga wanyama usiku, kuwinda wanyama bila kujali umri, kupiga wanyama nje ya maeneo waliyopewa), kukutolipa tozo mbalimbali za maendeleo za jamii kwenye vijiji jirani na maeneo wanaoendesha biashara ya uwindaji, kushindwa kuendesha ipasavyo shughuli za kuzuia ujangili.

Dk. Kigwangalla aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni ndugu Pasanis na wenzake ambao wanamilikia kampuni ya Berlette Safari Corporation Ltd na Ngugu Shein Ralgi na wakurugenzi wenzake wa kampuni ya Game Frontiers of Tanzania Ltd.

Wengine ni Ndugu Howel na wakurugenzi wenzake wa kampuni ya Mkwawa Hunting Sfaris Tanzania Ltd, Ndugu Thomas Fredikin na wenzake wa Kampuni ya Mwiba Holdings Ltd, Wengert Windrose Safaris Tanzania  Ltd na Tanzania Game Trackers Safaris Ltd, na Ndugu Awadh na wenzake ambao wanamiliki kampuni ya Uwindaji wa Greenmiles Safaris Ltd.

Aliwataja washirika wengine kuwa ni Ndugu ni Kwizema, Ndugu Robert, Ndugu Solomon Makulu, Ndugu Siasa Shaban, Ndugu Hamis Abdul Ligagabile na mtumishi wa Wizara Wizara ya Maliasili na Utalii, Alex Aguma.

Katika hatua nyingine Dk. Kigwangalla ametoa Ilani ya siku 30 kwa watu mbalimbali ikiwemo Mawaziri Wakuu Wastaafu waliovamia kiwanja chenye hati namba 4091 kilichopo Njiro Jijini Arusha wafike kwa Kamishna Mkuu wa Ardhi waweze kuhakikiwa na kuthibitisha umiliki wao halali ama sivyo wavirejeshe Serikalini viweze kumilikishwa kwa mmiliki wake halali.

“Natoa ilani ya siku 30 kwa mtu yeyote ambaye anajua alivamia kiwanja katika eneo hili ambalo lina hati namba 4091 kilichopo Njiro, Arusha, haraka sana ajipange kupeleka taarifa zake mbele ya Kamishna wa Ardhi kabla hatujachukua hatua nyingine za kisheria, hati iliyoko pale ipo katika jina la Bodi ya Utalii Tanzania japo wao wanadai wana hati nyingine.

“Wengi wao wamejenga nyumba za kudumu katika eneo lile, na wengine ni viongozi waliokuwa mawaziri wakuu wastaafu nao wana viwanja katika eneo hilo na wamejenga nyumba zao katika eneo hilo,” alisema Dk. Kigwangalla.

Alisema kiwanja hicho kilichokuwa na ekari zaidi ya 40 kilikuwa kinamilikiwa na taasisi ya Serikali ambayo ni kampuni tanzu ya Bodi ya Utalii Tanzania iliyokuwa inajulikana kama Serengeti Safari Lodges na baadae kikauzwa kwa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro.

Wakati huo huo, Dk. Kigwangalla ametoa siku saba kwa Jeshi la Polisi nchini kuchukua hatua dhidi ya watuhumiwa wanne wanaojihusisha na mtandao wa ujangili pamoja na kupanga njama zilizopelekea mauaji ya Mhifadhi wa Wanyamapori Ndugu Wayne Lotter, raia wa Afrika ya Kusini ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Kampuni Pams Foundation, aliyeuawawa eneo la Chole Masaki Jijini Dar es Salaam mwezi Agosti mwaka jana.

“Natoa siku saba kwa wenzetu wa jeshi la Polisi wachukue hatua dhidi ya watu wanne, ambao mimi majina yao ninayafahamu ambao miongoni mwao watatu wanahusika na kuendesha biashara ya ujangili, na ni watu wakubwa, ni matajiri wakubwa na wana mitandao mikubwa ya ujangili.

“Ninafahamu taarifa hizi polisi wanazo lakini hawajachukua hatua za kuwakamata watu hawa na kuwafikisha kwenye macho ya sheria, muda ni mrefu  na sisi wenye taarifa hizi sasa tumeanza kuchoka kusubiri.

“Hawa watu wanne walihusika kupanga njama ambazo zilipelekea kusababisha mauaji ya kikatili ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Palm Foundation, Ndugu Wayle Lotter mwezi Agosti mwaka jana eneo la Chole Masaki mwezi Agosti mwaka jana.

“Nataka ndani ya siku hizi saba wawe wamechukua hatua na kama hawatochukua hatua manaake tutajua wana vested interest (maslahi) kwahivo tutaenda kuripoti kwa Amiri Jeshi mkuu ambaye ni Mhe. Rais aliyetutuma kazi ya kusimamia sekta hii,”. Alisema Dk. Kigwangalla.
 Dk. Kigwangalla akizungumza katika mkutano huo leo mjini Dodoma.
Posted by MROKI On Friday, January 26, 2018 No comments

January 25, 2018

 Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina masenza akiongea na maafisa watendaji wa wilaya ya kilolo kwa lengo la kuhimiza ufanyaji kazi wao kwa kutatua changamoto za wananchi na hatimaye wapate maendeleo
pichani ni baadhi ya maafisa watendaji wa vijiji,kata na tarafa waliohudhuria kikao hicho cha mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza
Na Fredy Mgunda, Iringa.
MKUU wa mkoa wa Iringa Amina Masenza amewataka watendaji wote wa serikali kuacha kufanya kazi kwa mihemuko ya kisiasa kwa kuwa linarudisha maendeleo nyuma.
 
Onyo hilo limetolewa wakati wa kikao na maafisa watendaji wa wilaya ya Kilolo,Masenza alisema kuwa imebuka tabia ya viongozi wa serikali kujihusisha na siasa wakati wa utendaji wao wa kazi hivyo kuanzia saizi zitaki kusikia siasa wakati wa kazi.

“Haiwezekani kila siku mnafanya siasa tu huko vijijini badala ya kutengeneza mpango kazi wa kimaendeleo ambao utakuwa na faida kwa taifa na wananchi wote hivyo kuanzia leo sitaki kusikia tena hiyo tabia” alisema Masenza

Masenza alisema serikali ya awamu ya tano inataka watu wafanye kazi hivyo wakati siasa hakuna tena kama kuna viongozi wanataka siasa wasubili wakati ukifika watafanya hizo siasa.

“Jamani rais wetu ameshasema kuwa huu sio wakati wa porojo za kisiasa huko makazini hivyo mnapaswa kufanya kazi na sio kupiga siasa fanyeni kazi kwa nguvu zote kuhakikisha mnatatua kero za wananchi katika maeneo yenu husika” alisema Masenza

Masenza alisema kama kuna mtendaji wa serikali anataka kufanya kazi za kisiasa basi hana budi kuachia nafasi yake ya kazi ili akaendelee kufanya kazi ya siasa na nafasi yake itajazwa na viongozi ambao wapo tayari kufanya kazi na serikali ya awamu ya tano.

Aidha Masenza aliwaagiza wakurugenzi wote mkoani Iringa kuwachukulia hatua za kisheria mara moja viongozi wa serikali watakuwa wanajishughulisha na maswala ya kisiasa la sivyo wao ndio watachukuliwa hatua kwa kufuata miongozo ya kiserikali inavyoagiza.

“ wakurugenzi mnawajua sana hawa watendaji hivyo ni lazima muwadhibiti kufanya siasa wakati wa kazi na mnatakiwa kuwa wakali pindi mtakapogundua kuwa wanafanya siasa makazini” alisema Masenza

Naye katibu tawala wa mkoa wa Iringa Wamoja Ayubu alisema kuwa ameshatoa walaka unaonyesha majukumu ya watendaji wa serikali hivyo hategemee kuona kiongozi wa serikali akifanya siasa kazini.

“Jamani nimetuma na kuwa walaka wa majukumu yenu hivyo sitegemie mnakiuka la sivyo nitaanza kuwa sughulikia kiongozi mmoja mmoja ili nikomeshe tatizo la siasa makazini” alisema Ayubu

Ayubu aliwataka makatibu wa wilaya kufanya kazi kwa kufuata miongozo ya serikali la sivyo serikali haitafikia malengo ya kuleta maendeleo kwa wananchi kama ambavyo wamejipangia hivyo inapaswa  kila mmoja anafanye majukumu yake kikamilifu ili kutimiza malengo ya serikali.

“Rais wa awamu ya tano DR John Pombe Magufuli hataki tufanye kazi kimazoea kama ambavyo ili kuwa awali saizi ni kazi tu hivyo ni lazima kufanya hivyo” alisema Ayubu

Posted by MROKI On Thursday, January 25, 2018 No comments
Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi akizungumza kwenye kikao cha wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Mazingira iliyofanya ziara ya kikazi kwenye Hifadhi ya Taifa Ziwa Manyara mkoa wa Arusha,kulia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Japhet Hasunga. 
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Millanzi akizungumza kwenye kikao na kamati hiyo,kushoto ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Japhet Hasunga na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo,Kemilembe Lwota akifatilia kwa makini. 
Mbunge wa jimbo la Sumve mkoa wa Mwanza,Richard Ndassa(kushoto),Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Japhet Hasunga(katikati) na Meneja Mawasiliano wa Tanapa,Pascal Shelutete wakiwa ndani ya Hifadhi hiyo. 
Meneja Ujirani Mwema wa Tanapa,Hemed Mbugi akitembea juu ya daraja linalo ‘bembea’ ambalo ni moja kivutio kwa watalii wa nje na ndani. 
Mbunge wa jimbo la Mtama mkoa wa Lindi akifurahia daraja linalo ‘bembea’ ambalo ni moja kivutio kwa watalii wa nje ya nchi na ndani. 
Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Kemilembe Lwota akitembea juu ya daraja hilo. 
Meneja Mawasiliano wa Tanapa,Pascal Shelutete naye hakua nyuma kutembea juu ya daraja hilo ambalo limeongeza shughuli za utalii kwenye hifadhi hiyo. 
Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Mazingira wakiwa juu ya daraja maalumu lililojengwa kuwawezesha watalii kuwaona wanyama aina ya Viboko na aina mbalimbali za ndege. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Japhet Hasunga akifurahia mandhari ya daraja linalomwezesha mtalii kuona vizuri eneo la Ziwa Manyara. 


Posted by MROKI On Thursday, January 25, 2018 No comments
Wafanyakazi na uongozi wa Jeshi la Uhamiaji wakiwa wameshika mfano wa ufunguo baada ya makabidhiano ya nyumba 63 za makazi katika mradi wa Iyumbu Satellite Center. Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limekabidhi nyumba za makazi zilizojengwa kwenye mradi wa kitovu cha mji wa kisasa wa nyumba za gharama nafuu wa Iyumbu Satellite Centre kwa Idara ya Uhamiaji.Meneja wa Masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa, Itandula Gambalagi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa na Kamishna wa Fedha, Ndugu Peter Chogero kwa niaba ya Kamishna Mkuu wa Uhamiaji wakikabidhiana hati ya makabidhiano ya nyumba baada ya kukabidhi nyumba 63 kwa Jeshi la Uhamiaji.
Picha ya pamoja ya uongozi wa Shirika la Nyumba na Uhamiaji baada ya makabidhiano ya nyumba 63 za makazi katika mradi wa Iyumbu Satellite Center. Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limekabidhi nyumba za makazi zilizojengwa kwenye mradi wa kitovu cha mji wa kisasa wa nyumba za gharama nafuu wa Iyumbu Satellite Centre kwa Idara ya Uhamiaji.
Picha ya pamoja ya uongozi wa Shirika la Nyumba na Uhamiaji baada ya makabidhiano ya nyumba 63 za makazi katika mradi wa Iyumbu Satellite Center. Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limekabidhi nyumba za makazi zilizojengwa kwenye mradi wa kitovu cha mji wa kisasa wa nyumba za gharama nafuu wa Iyumbu Satellite Centre kwa Idara ya Uhamiaji.
****************
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)  limekabidhi nyumba za makazi zilizojengwa kwenye mradi wa kitovu cha mji wa kisasa wa nyumba za gharama nafuu wa Iyumbu Satellite Centre kwa Idara ya Uhamiaji. 

Mradi huu ambao ujenzi wake ulianza Desemba 2016 una ukubwa wa ekari 234 na ni moja ya sehemu ya mji uliopangiliwa kitaalamu kwa kuzingatia sheria na kanuni za mipango miji na utajengwa katika awamu tatu. Nyumba hizi 63 ambazo zimeshakamilika na kuanza kukaliwa zinakabidhiwa leo kwa Idara ya Uhamiaji.

Makabidhiano haya yamefanywa na Meneja Masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa, Ndugu Itandula Gambalagi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NHC na Kamishna wa Fedha, Ndugu Peter Chogero kwa niaba ya Kamishna Mkuu wa Uhamiaji.

Makabidhiano haya yanafanyika baada ya ahadi ya Shirika la Nyumba kwa Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli ya kujenga nyumba makao makuu ya nchi Dodoma.

Katika uzinduzi wa nyumba hizi, Mkurugenzi Mkuu wa NHC alimhakikishia Mh. Rais kwamba nyumba hizi zimekamilika na ziko tayari kwa kukaliwa.

Leo ni siku ya furaha kuona kwamba NHC inakabidhi nyumba kwa Uhamiaji ambaye ni mmoja wa wanunuzi wakubwa wa nyumba katika mradi huu.

Nyumba hizi ni bora kabisa zimejengwa kwa ustadi mkubwa. Ni wito wetu kwamba nyumba hizi watazitunza ikiwa na mazingira yake.

Mradi huu wa nyumba 300 ikiwa 150 zimekamilika ni kati ya miradi mingi ambayo NHC inatekeleza.
Posted by MROKI On Thursday, January 25, 2018 No comments
MIGOGORO ya ardhi ni miongoni mua vitu ambavyo vimekuwa vikirudisha sana maendeleo nyuma.

Mara nyingi migogoro hiyo husababisha kusimama kwa shughuli mbalimbali za amendes kama ujenzi na kubwa zaidi shughuli za kilimo kwa wananchi wa maeneo husika hasa maeneo ya vijijini amber hutegemea arch kwa kuzalisha chakula.

Chalinze ni moja ya Halmashauri za Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani ambazo zinakabiliwa na migogoro kadhaa ya ardhi. 

Miongoni mwah migogoro hiyo ni ule uliopo katika Kijiji cha Kwamduma Kata ya Kibindu, amber ni baissa ya kijiji hicho na Hifadhi ya Uzigua.

Katika kutafuta utatuzi wa migogoro hiyo, Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete alitembelea kijiji cha Kwamduma ili kuona namna ya kutatua agogo huh wa muda mrefu vaina ya Kijiji na Hifadhi.

Ridhiwani alisema lingo la tiara hiyo ni kuangalia athari za migogoro ya arch Latina kijiji Nicholas na kuzitafutia ufumbuzi baina ya wananchi na hifadhi".

"Nimefanya Ziara katika kijiji cha Kwamduma, Kata ya Kibindu kuangalia Athari za Migogoro Baina ya Kijiji na Hifadhi ya Uzigua, katika ziara hiyo tumeona hitaji la kukaa chini na watu wa hifadhi na kujadili suala la mipaka inayotembea,"alisema Ridhiwani. 

Alisema kuwa wamekubaliana na Serikali kuingilia kati mgogoro huo na kuutafutia ufumbuzi wa haraka.

"nashukuru Serikali imekubali kuushughulikia mgogoro huu kwa baraka ndani ya kipindi kifupi, ili shughuli nyingine za maendeleo ziendelee,"alisema Ridhiwani.
Posted by MROKI On Thursday, January 25, 2018 No comments

January 24, 2018

Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua moja ya shule ya sekondari ambayo inajengwa kwa nguvu za wananchi na serikali kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu mkoani Iringa
 Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua moja ya shule ya sekondari na akiuliza kitu kuhusu ujenzi wa shule ya sekondari ya Nyanzwa
 Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua moja ya shule ya sekondari akielekea kukagua vyoo vya shule ya sekondari ya Nyanzwa.
 Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua vyoo vya shule ya Nyanzwa. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Posted by MROKI On Wednesday, January 24, 2018 No comments
  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo