Nafasi Ya Matangazo

June 10, 2017

1
Mkurugenzi wa Kampuni ya Candy And Candy Bw. Joe Kariuki akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelelzo leo wakati akitambulisha Aplication yake mpya kwa ajili ya kuuza Vyakula, Vinywaji na Filamu Movie leo, kushoto ni Meneja wa kampuni hiyo Bi Hasna Mwishehe.
2
Mkurugenzi wa Kampuni ya Candy And Candy Bw. Joe Kariuki akionyesha Aplication hiyo jinsi inavyofanya kazi wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelelzo leo wakati akitambulisha Aplication yake mpya kwa ajili ya kuuza Vyakula, Vinywaji na Filamu Movie leo, kushoto ni Meneja wa kampuni hiyo Bi Hasna Mwishehe.
3
Mkurugenzi wa Kampuni ya Candy And Candy Bw. Joe Kariuki akizmpigia simu mmoja wa wamiliki wa mgahawa ulioko Sinza na kuagiza chakula ili aletewe alipo wakati akitambulisha Aplication yake mpya kwa ajili ya kuuza Vyakula, Vinywaji na Filamu Movie leo, kushoto ni Meneja wa kampuni hiyo, Hasna Mwishehe.
***************
Kwa mara ya kwanza kampuni ya Candy and Candy imeanzisha Application mpya inayojulikana kama NIKO HUB ambayo ni mkombozi wa wafanyabiashara wengi na watumiaji wa mtandao huo.NIKO HUB inajihusisha na mambo yote yanayohusu vyakula,vinywaji na filamu (movies).
Lengo kubwa la NIKO HUB ni kunyanyua wafanyabiashara wakubwa na wadogo kwa kupanua soko lao na kujiongezea kipato zaidi zaidi na kumuondolea usumbufu mteja wakati anapohitaji huduma ambapo Aplication hii inamfanya mteja kuagiza bidhaa na kuletewa mahali alipo kikubwa anachotakiwa kufanya ni kupakua Aplication hii kwenye Google Play bure na kisha anaanza kuitumia kwenye simu yake.
NIKO HUB inafanya kazi mahali popote ulipo katika bara la Afrika na popote unapoenda huhitaji kupakua Aplication nyingine bali unaendelea kutumia ileile, Aplication hii pia inabadili lugha kulingana na lugha inayotumika katika nchi husika kwa mfano Tanzania inapatikana kwa kiswahili lakini ukienda kwenye nchi za kiarabu zilizoko Afrika itakuletea lugha ya kiarabu na ukienda nchi inayotumia lugha ya kifaransa itafanya hivyo pia N.K
Jambo kubwa ni kwamba NIKO HUB pia imeandaa tamasha litakalojulikana kama NIKO HUB EAT OUT FESTIVAL ambalo litafanyika siku ya sikukuu ya Eid na hakutakuwa na kiingilio kwa washiriki ambapo litashirikisha wajasiriamali mbalimbali wanaojihusisha na uuzaji wa vyakula mbalimbali na vinywaji
Tamasha hilo litafanyika jijini Dar es salaam kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni na litajumuisha burudani mbalimbali huku wasanii kadhaa wakitumbuiza kwenye tamasha hilo.
Tamasha hilo pia kutakuwa na michezo ya watoto ambapo wazazi na walezi watapata fursa ya kujumuika pamoja na familiazao .
Aidha kutakua na mafunzo mbalimbali kwa ajili ya kuboresha biashara zao.Kupitia NIKO HUB EAT OUT FESTIVAL huku watoto wakifundishwa kuishi katika mazingira ya usafi kwa ajili ya afya zao.
Kampuni ya Candy n Candy iliyoanzishwa rasmi mwaka 2014 chini ya uongozi wa Joe Kariuki, ambayo ni kampuni Tanzu ya makampuni ya Candy and Candy Records, Candy Air, Candy Mining, Candy Rhythm Night Club na The evening Post Blog,Baabkubwa pamoja na Big ishu yameingia kwenye soko na kuleta mageuzi katika biashara.
Kampuni ya Candy Records imewahi kufanya kazi na wasanii wengi wa ndani na nje ya nchi ya Tanzania wakiwemo Mr Nice, Baby Madaha, Top C, Fat S,Hussein Machozi na wengine wengi.
Posted by MROKI On Saturday, June 10, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo