Mwanariadha Alphonce Simbu aliyeshika nafasi ya
tano katika mashindano ya London Marathon anatarajia kutembelea Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Alhamisi April 27 akiwa ni mgeni maalum
wa Waziri wa Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni
Harison Mwakyembe.
Baada ya kutembelea Bunge hilo Simbu pia atakuwa na
mazungumzo na Waziri Mwakyembe.
Simbu ataambatana na muwakilishi wa wadhamini wake DStv pamoja na maafisa waandamizi wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT.
Akizungumzia mualiko huo, mwanariadha huyo amesema
kuwa amefurahi sana kupata mualiko wa Waziri anayehusika na sekta ya
michezo kwenda bungeni kama mgeni wake maalum.
Amesema hii inaonyesha
kuwa serikali inatambua jitihada zake anazozifanya
katika kuiwakilisha vyema nchi katika mashindano ya kimataifa.
“Nimefurahi sana kualikwa na muheshimiwa Waziri kumtembelea bungeni,
bila shaka hii itakuwa fursa nzuri ya hata wabunge kutambua jitihada
tunazofanya vijana wao katika kuliletea taifa sifa.
Natumaini
pia nitapata fursa ya kuongea ana kwa ana na Waziri” alisema Simbu na
kuongeza kuwa atatumia fursa hiyo kumueleza Waziri changamoto nyingi
wanazokabiliana nazo wanamichezo hapa nchini.
Amesema kuna mengi ya kuongea na Waziri na kwamba
anaamini mazungumzo yao yatakuwa na tija na manufaa si kwake tu, bali
kwa wanamichezo wote kwa ujumla.
Kwa upande wake, Meneja Uhusiano wa Multichoice
Tanzania Johnson Mshana, ambaye anaandamana na Simbu, amesema kuwa
anaamini kuwa ziara hiyo na mkutano na Waziri utakuwa na manufaa makubwa
kwani pia itakuwa ni fursa nzuri ya kujadili namna
bora zaidi ya Serikali kushirikiana na wadau katika kuimarisha na
kuendeleza michezo hapa nchini.
“sisi kama wadhamini wa mwanariadha huyu
tunaamini kuwa kitendo cha Waziri kutualika ni ishara tosha kuwa kweli
anadhamiria kushirikiana na sisi wadau wa michezo
ili kuongeza nguvu za pamoja za kuimarisha michezo hapa nchini” alisema
Mshana
Multichoice Tanzania kupitia DStv imekuwa
ikimdhamini Simbu tangu mwaka jana na udhamini huo pia umewanufaisha
wanariadha wengine ambao wamekuwa kambini kwa muda sasa pamoja na simbu.
“Kambi ya mazoezi ya Simbu ambayo ilidhaminiwa na DStv
pia ilikuwa na wanariadha wengine ambao wote walinufaika moja kwa moja
na udhamini huo. Tunaamini kuwa pia kati ya hao tutapata wanariadha
watakaofanya vizuri siku zijazo”.
Alphonce Simbu, ambaye pia ni mshindi wa medali ya
dhahabu katika mashindano ya Mumbai Marathon ni miongoni mwa wanariadha
wa timu ya Taifa itakayoshiriki katik mashindano ya Dunia yatakayofanika
jijini London mwezi Agosti mwaka uu
0 comments:
Post a Comment