Meneja wa kiwanda cha TBL Mbeya,Jemedari Waziri
akiwakabidhi kombe la ushindi baadhi ya wafanyakazi waliofika uwanja wa ndege
wa Songwe kumpokea akitokea nchini Afrika ya Kusini.
Mwonekano wa kombe la ushindi
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Mbeya wakiangalia
kombe la ushindi
Meneja Rasilimali watu wa kiwanda cha Bia cha
TBL- Mbeya, Sarah Zayumba (aliyeshika kombe), akiwa ameshika kombe hilo
baada ya kuwasili katika kiwanda hicho.
Baadhi ya Wafanyakazi wa
Kiwanda cha Bia cha TBL- Mbeya, wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa na kombe
na cheti cha ushindi baada ya kiwanda hicho kutwaa tuzo ya kuwa kiwanda
bora na kushika nafasi ya kwanza Afrika kati ya viwanda 21 vya bia barani
Afrika muda mfupi baada ya Meneja wa Kiwanda hicho, Jemedari Waziri kuwasili
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe (SIA)-Mbeya akitokea Afrika ya
Kusini. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
**************
WAKATI serikali ya awamu ya tano inajipanga
kuifanya Tanzania nchi ya viwanda tayari dalili njema zimeishajitokeza kuwa
watanzania tukiamua tunaweza kwa kuwa kiwanda kinachoshikilia rekodi ya ubora
barani Afrika ni kiwanda cha kutengeneza Bia cha TBL kilichopo katika kitongoji
cha Iyunga mkoani Mbeya.
Kwa mara nyingine tena baada ya kushindanishwa
na viwanda vikubwa vipatavyo 21 barani Afrika,mwishoni mwa wiki iliyopita
TBL Mbeya imeibuka kinara na kutangazwa kuwa kiwanda bora barani Afrika kati ya
viwanda vilivyopo chini ya kampuni kubwa yenye viwanda vya kutengeneza bia
duniani ya SABMiller na kimelinda rekodi yake kilichokuwa kinaishikilia.
Rekodi hii inaenda sambamba na dhamira ya
serikali ya kuifanya Tanzania nchi ya viwanda na inadhihirisha kuwa uwekezaji
wa viwanda sio lazima ufanywe maeneo ya mijini kama ambavyo ilikuwa imezoeleka
kwa muda mrefu.
Mhandisi Jemedari Waziri,Meneja wa kiwanda hiki
akiongelea mafanikio haya alisema kuwa anajivunia ushindi huu kwa kuwa ni
uthibitisho halisi kuwa watanzania tunaweza kufanya vizuri na kuleta
maendeleo kwa kasi tukiamua.
“Tunaposema ubora wa kiwanda tunaamaanisha ubora
wa bidhaa tunazozalisha,teknolojia tunazotumia,raslimali watu
tuliyonayo,mchango wa kiwanda kwa serikali na jamii iliyotuzunguka bila kusahau
utunzaji wa mazingira ambayo ni moja ya nguzo ya kampuni yetu”.Alisema.
Aliongeza kuwa ushindi huu ni kwa wana Mbeya
wote na wana kanda ya Nyanda za Juu Kusini “Tunawashukuru wateja wetu wote kwa
kutuunga mkono wakati wote na tutaendelea kuwaletea bidhaa bora kwenye soko na
kubuni miradi mbalimbali ya kijamii itakayosaidia kuleta mabadiliko”.Alisema
Jemedari pia alisema ushindi huu unatokana na
jitihada za pamoja kutoka kwa wafanyakazi wote wa kiwanda na TBL Group kwa
jumla na anafurahi kuona kiwanda kinaendeshwa na watanzania asilimia kubwa
ikiwa ni vijana wenye vipaji vya ajabu na waliobobea katika fani mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment