Mkuu wa wilaya ya mufindi Jumhuri Wiliamu akipiga mpira katika eneo la penati kuashiria kuwa mashindano ya mgimwa cup yamezinduliwa rasmi
Mkuu wa wilaya mufindi Jumhuri Wiliamu aliyeshika mpira kulia sambamba na mwenyekiti wa ccm mufindi yohanis kaguo aliyeshika mpira kushoto wakiwa na baadhi ya wachezaji
Mkuu wa wilaya mufind Jumhuri Wiliamu akikagua timu kabla mtanange kuanza.
Mkuu wa wilaya mufind Jumhuri Wiliamu akikagua timu kabla mtanange kuanza huku akiwapa neno wachezaji wa timu husika katika kiwanja cha Ikwea.
Akizindua mashindano hayo
yaliyofanyika Kiwanja cha Ikwea katika kijiji cha Ikwea mkuu wa wilaya Jumhuri
Wiliamu kwa niaba ya Mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini alisema ni wakati
mzuri kwa sasa kuyageukia mashindano ya mchangani kwani yamesheheni vipaji
vingi vitakavyosaidia kuendeleza mpira wa Tanzania wakati ambapo taifa
likiendelea kupata matokeo yasiyoridhishwa kwenye soka kwa sasa,
"Mashindano haya ni
muhimu sana kwa wakati huu kwani yatasaidia kuinua vipaji vya vijana wetu na
kuweza kupata timu bora ya taifa hivyo nidhamu ni muhimu wakati wa michezo
hiyo" alisema Wiliamu
Aidha Wiliamu aliongeza kwa
kusema kuwa mpira wa miguu umekuwa na faida kwa wachezaji kwani wanaweza
kujitengezea vyanzo vya ajira kama mbwana samatta na wachezaji wengine walipwa
vizuri saizi hapa nchini hata nje ya nchi.
“ Soka imewapa ajira mamilioni ya wachezaji na
viongozi ulimwenguni na wameweza kuishi maisha ya kifahari kutokana na
mishahara wanayopata”, alisema Wiliamu
Mwenyekiti wa Kamati ya
Mashindano hayo Felix nyimbo aliwataka washiriki wa mashindano hayo kujituma
ili ipatikane timu ya kata ambayo itakuwa ikiwakilisha kata hiyo katika
mashindano ya wilaya, kanda hadi taifa.
“Mwaka huu tumekuja na
wataalamu wanachagua vipaji maalumu kwaajili ya kujiunga na timu yetu ya
kurugenzi ya mafinga na lengo likiwa ni kuhakikisha vipaji vyote vya jimbo la
mufindi kaskazini vinaonekana na vinafika mbali kwa kuwa sasa mpira ni ajira si
mnamuana mchezaji Mbwana Samatta”.alisema nyimbo
Kwa upande wake mlezi wa
mashindano hayo mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (ccm) wilaya mufindi Yohanes
Kaguo alisema ataendelea kwaunganisha vijana kupitia michezo na kusaidia kukuza
mpira wa wilaya ya mufindi.
“Ilani ya chama cha
mapinduzi inatutaka mwenyeviti kote nchini kuhakikisha michezo inafanyika mara
kwa mara na kuleta tija kwa taifa ili tuondokane kuwa kuwa vichwa vya
wendawazimu”alisema kaguo.
Mashindano ya mgimwa Cup ni
miongoni mwa mashindano yanayolenga kuibua vipaji vya vijana vijijini ili
kuwawezesha kupata nafasi ya kucheza katika vilabu vikubwa nchini.
0 comments:
Post a Comment