Nafasi Ya Matangazo
Showing posts with label UCHUMI. Show all posts
Showing posts with label UCHUMI. Show all posts

September 16, 2022

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (katikati), Mkuu wa Masuluhisho ya Mikopo kwa Afrika kutoka Investec Bank, Rowan King (wapili kulia), Mkurugenzi wa Huduma za Mikopo ya Pamoja wa Benki ya Intesa Sanpaolo, Gustaaf Eerenstein (kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Benki Kimataifa wa Bank One, Carl Chirwa (wapili kushoto) pamoja na Meneja Mikopo Maalum Benki ya Biashara ya Mauritius,Hans Dallo wakiweka mikono pamoja ikiwa ni ishara ya kuonyesha ushirikiano baada ya kusaini mikataba ya makubaliano waliyosaini inayoiwezesha Benki ya CRDB kupata kiasi cha dola za kimarekani milioni 130 kwa ajili ya kukopesha sekta za biashara na wajasiriamali nchini.
---
Benki ya CRDB leo imeingia mkataba wa makubaliano na Benki ya kimataifa ya Intesa Sanapaolo ya nchini Italia, na Investec Bank ya nchini Afrika Kusini unaoiwezesha benki hiyo kupata kiasi cha dola za kimarekani milioni 130 kwa ajili ya kukopesha sekta za biashara na wajasiriamali nchini.

Mapema mwaka huu, Benki ya CRDB iliingia mkataba wa awali na benki hizo za kimataifa kusaidia kupatikana fedha katika masoko ya kimataifa kwa ajili ya kuimarisha mtaji wa benki hiyo na kukuza uwezo wa kutoa mikopo.

“Tunafurahia sana kufanikisha makubaliano haya. Fedha hizi zilizopatikana kutoka masoko ya kimataifa zitasaidia kuimarisha mtaji wa Benki yetu na kukuza uwezo wetu wa kutoa mikopo kwa wateja wakubwa na wadogo hapa Tanzania na Burundi. Kipekee niwashukuru Investec Bank na Intesa Sanpaolo kwa ushirikiano waliotupa,” alisema Abdulmajid Nsekela, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB.
Benki ya CRDB inakuwa benki ya kwanza nchini kupata fedha za uwekezaji kutoka masoko ya kimataifa. Kwa mujibu wa Nsekela, lengo lilikuwa ni kukusanya dola milioni 50, lakini viwango bora na ufanisi mkubwa wa benki hiyo ulivutia wawekezaji wengi wa kimataifa, na kupelekea kupatikana kwa dola milioni 130.

Benki ya CRDB ni moja ya benki kumi zilizoorodheshwa kama benki bora na salama zaidi kuwekeza barani Afrika na Moody`s Investors Services na kupewa daraja la ‘B1 Outlook” ambalo ni daraja la juu zaidi kwa taasisi za fedha katika ukanda wa jangwa la Sahara. Mwaka huu Benki hiyo pia imetajwa kuwa ’Benki Bora Tanzania’ na jarida maarufu la nchini Uingereza.

“Kama Benki inayoongoza nchini Tanzania, Benki ya CRDB inaendelea kutazama fursa za biashara katika sekta za kimkakati ili kukuza uchumi wa nchi. Fedha hizi zitatusaidia kuimarisha shughuli zetu za utoaji mikopo hususani mikopo ya wanawake na vijana na kuimarisha zaidi nafasi yetu katika soko kama benki inayoongoza kwa kufadhili sekta za uchumi,” aliongeza.
Rowan King, Mkuu wa Masuluhisho ya Mikopo kwa Afrika kutoka Investec Bank, alisema kupatikana kwa fedha hizo katika masoko ya kimataifa kunaonyesha ni imani ya taasisi za fedha duniani kwa Benki ya CRDB na uchumi wa Tanzania.

"Tanzania imeonekana kuwa sehemu muhimu ya hadithi ya ukuaji wa Afrika katika miaka michache iliyopita. Bidhaa nyingi muhimu zinazozalishwa Afrika Mashariki, zinasafirishwa nje ya nchi kupitia bandari za Tanzania. Tanzania ina jukumu muhimu katika biashara katika kuimarisha biashara baina ya nchi za Afrika,” alisema.
Dola milioni 130 zilizopatikana ni mara mbili na nusu ya kiasi kilichokusudiwa, anasema Gustaaf Eerenstein, Mkurugenzi wa Huduma za Mikopo ya Pamoja Investec Bank. "Hii inaonyesha kiwango cha juu cha imani ambayo wawekezaji wanayo kwa Benki ya CRDB," alisema Eerenstein.

Ushirikiano huu na Benki ya CRDB na benki za Intesa Sanpaolo na Investec unaendelea kuimarisha uwezo wa benki hiyo katika kutoa mikopo, ambapo mwaka huu pekee imeweza kuingia makubaliano ya zaidi ya Dola za Kimarekani Milioni 300 na mashirika kama IFC, AFDB, AGF, PROPARCO, USAID na DFC kwa ajili ya uwezeshaji wa biashara ndogo na za kati (SME), na uwezeshaji wa kiuchumi kwa wanawake na sekta zisizo rasmi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (katikati), Mkuu wa Masuluhisho ya Mikopo kwa Afrika kutoka Investec Bank, Rowan King (wapili kulia), Mkurugenzi wa Huduma za Mikopo ya Pamoja wa Benki ya Intesa Sanpaolo, Gustaaf Eerenstein (kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Benki Kimataifa wa Bank One, Carl Chirwa (wapili kushoto), na Meneja Mikopo Maalum Benki ya Biashara ya Mauritius,Hans Dallo wakionyesha mikataba ya makubaliano waliyosaini inayoiwezesha Benki ya CRDB kupata kiasi cha dola za kimarekani milioni 130 kwa ajili ya kukopesha sekta za biashara na wajasiriamali nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kushoto), Mkuu wa Masuluhisho ya Mikopo kwa Afrika kutoka Investec Bank, Rowan King (wapili kulia), Mkurugenzi wa Huduma za Mikopo ya Pamoja wa Benki ya Intesa Sanpaolo, Gustaaf Eerenstein (wapili kushoto), na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Benki Kimataifa wa Bank One, Carl Chirwa wakisaini mkataba wa makubaliano unaoiwezesha Benki ya CRDB kupata kiasi cha dola za kimarekani milioni 130 kwa ajili ya kukopesha sekta za biashara kwa wajasiriamali nchini katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Benki ya CRDB, jijini Dar es Salaam leo tarehe 15 Septemba 2022.

Posted by MROKI On Friday, September 16, 2022 No comments

September 02, 2022

MENEJA  wa Benki ya CRDB Kanda ya Kati,Chabu Mishwaro,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Promosheni Maalum ya Matumizi ya Kadi iliyopewa jina la ''Tisha na TemboCard'' kwa Kanda ya Kati iliyofanyika leo Septemba 2,2022 jijini Dodoma.
MENEJA wa Biashara Kanda ya Kati Jane Maganga,akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Promosheni Maalum ya Matumizi ya Kadi iliyopewa jina la ''Tisha na TemboCard'' kwa Kanda ya Kati iliyofanyika leo Septemba 2,2022 jijini Dodoma.
MENEJA  wa Benki ya CRDB Kanda ya Kati,Chabu Mishwaro (Kusoto) akizindua  Promosheni Maalum ya Matumizi ya Kadi iliyopewa jina la ''Tisha na TemboCard'' kwa Kanda ya Kati.Kulia ni Meneja Mwandamizi Malipo ya Kadi kutoka CRDB Bw.Victor Makere hafla iliyofanyika leo Septemba 2,2022 jijini Dodoma.
 
MENEJA Mwandamizi Kitengo cha Kadi kutoka CRDB Bw.Karington Chahe,akielezea jinsi promosheni hiyo itakavyokuwa inafanyika mara baada ya kuzinduliwa kwa Promosheni Maalum ya Matumizi ya Kadi iliyopewa jina la ''Tisha na TemboCard'' kwa Kanda ya Kati iliyofanyika leo Septemba 2,2022 jijini Dodoma. Dodoma.
MTEJA wa CRDB Husna Mchana,ambaye ni mhudumu kutoka Kampuni ya Afroil Investment Pump,akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Promosheni Maalum ya Matumizi ya Kadi iliyopewa jina la ''Tisha na TemboCard'' kwa Kanda ya Kati iliyofanyika leo Septemba 2,2022 jijini Dodoma.
MENEJA  wa Benki ya CRDB Kanda ya Kati,Chabu Mishwaro,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua  Promosheni Maalum ya Matumizi ya Kadi iliyopewa jina la ''Tisha na TemboCard'' kwa Kanda ya Kati iliyofanyika leo Septemba 2,2022 jijini Dodoma.
MENEJA  wa Benki ya CRDB Kanda ya Kati,Chabu Mishwaro,akicheza burudani na wafanyakazi wa CRDB mara baada ya kuzindua  Promosheni Maalum ya Matumizi ya Kadi iliyopewa jina la ''Tisha na TemboCard'' kwa Kanda ya Kati iliyofanyika leo Septemba 2,2022 jijini Dodoma.
***************
BENKI ya CRDB imezindua  Promosheni maalum ya matumizi ya kadi iliyopewa jina la “Tisha na TemboCard” kwa Kanda ya Kati itakayoendeshwa kwa kipindi cha miezi 3 kuanzia ilivyozinduliwa rasmi Kitaifa jijini Dar-es-Salaam mnamo Agosti 18,mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo leo Septemba 2,2022 jijini Dodoma Meneja  wa Benki ya CRDB Kanda ya Kati,Chabu Mishwaro,amesema lengo la Promosheni hiyo ni kuwahamasisha wateja na Watanzania kujenga utamaduni wa kutumia kadi zao kufanya manunuzi na malipo ya huduma.

Bi.Mishwaro amesema kuwa  bado watanzania wengi hawana mwamko wa kutosha juu ya matumizi ya kadi.

“Promosheni hii ina lengo la kuwahamasisha wateja na watanzania kujenga utamaduni wa kutumia kadi zao kufanya manunuzi na malipo ya huduma huku wakijishindia zawadi,”amesema .

Aidha amezitaja  zawadi hizo ni fedha taslimu kila mwezi kwa wateja watatu ambapo watajishindia Sh.Milioni moja kwa mshindi wa kwanza, wengine washindi wawili watapata Sh.500,000 .

“Na kubwa zaidi ni safari ya kwenda nchini Qatar iliyolipiwa kila kitu kwa wateja wanne wa TemboCard, washindi ni wale tu watakaokuwa na miamala mingi kupitia kadi zao za TemboCard,”alisema.

Bi.Misharo amesema  kadi hizo zinatumika kupitia ATMs, matawi, CRDB Wakala, Mashine za malipo za (POS) na kufanya manunuzi na malipo kwa njia ya mtandao ndani na nje ya nchi.

''Ni matumaini yangu kuwa kampeni hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kujenga utamaduni wa watu kutumia kadi zao kufanya malipo na manunuzi.''amesema 

Hata hivyo amewasihi wateja wote wenye kadi za TemboCard kufurahia urahisi wa kufanya malipo popote pale walipo huku wakijiwekea nafasi ya kushinda zawadi.

 Amesema kuwa wateja ambao hawana akaunti katika Benki ya CRDB huu ndio wakati wa kufungua akaunti na kuanza kuweka fedha ili kurahisisha kufanya miamala kupitia TemboCard zao ambazo watapewa baada ya kufungua akaunti. 

Naye , Meneja Biashara Kanda ya Kati, Jane Maganga, amesema kuwa promosheni hiyo ni ubunifu wa CRDB katika kuwarahisishia wateja wake kupata huduma mbalimbali.

“Hii promosheni ya Tisha na TemboCard ni shindano ambalo litampa mabadiliko mteja, atakuwa akihitaji huduma au bidhaa anatumia kadi yake kuchanja tu na kulipia badala ya kutoa burungutu la fedha,”amesema Maganga
Posted by MROKI On Friday, September 02, 2022 No comments

 

Meneja wa Mawsiliano na Uhusiano wa Tanzania Commercial Bank (TCB) Gloria Mutta (wanne kulia), pamoja na Meneja Masoko wa Benki hiyo Dorothea Lymo wakiwaraki watoto wenye ulemavu wa akili wanaolelewa katika kituo kilichopo ndani ya shule ya msingi Bunju B walipokwenda kuwatembelea na kuwapa msaada wa mahitaji mbalimbali.
Meneja wa Mawsiliano na Uhusiano wa Tanzania Commercial Bank (TCB) Gloria Mutta (watatu kulia), akimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Wanafunzi wenye ulemavu wa  akili  kilichopo katika shule ya msingi Bunju B,  Gloria Mataba, wakati wa hafla ya benki ya TCB  ilipokwenda kutembelea kituo hicho nakutoa misaada ya vitu mbalimbali vya kibinadamu. Wengine pichani ni Mkuu wa kituo msaidizi Asaph Marere pamoja na wanafuzi hao.
Afisa Masoko wa  Tanzania Commercial Bank (TCB)   Dorothea Lymo, akikabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali ya kibinadamu ikiwemo Unga, sukari ,mafuta maziwa, mchele na vinginevyo kwa Mwenyekiti wa kituo hicho Salehe Athuman  cha  wanafunzi wenye ulemavu wa akili katika shule ya msingi Bunju B,  jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wa Mawsiliano na Uhusiano waTanzania Commercial Bank (TCB) Gloria Mutta, uongozi wa kituo hicho pamoja na wanafunzi hao hafla hiyo imefanyika leo shuleni hapo.
Meneja wa Mawsiliano na Uhusiano wa Tanzania Commercial Bank (TCB) Gloria Mutta (watano kulia) akikabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali ya kibinadamu ikiwemo Unga, sukari ,mafuta maziwa, mchele na vinginevyo kwa Mkuu wa Kitengo cha Wanafunzi wenye ulemavu wa  akili  kilichopo katika shule ya msingi Bunju B, jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni Afisa Masoko wa Benki hiyo Dorothea Lymo, watoto pamoja na Msaidizi wa Mkuu wa kituo hicho Asaph Marere. Hafla hiyo imefanyika leo shuleni hapo.


 

Posted by MROKI On Friday, September 02, 2022 No comments

July 07, 2021

 



Wananchi wakihudumiwa kwenye Banda la Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) katika Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayofanyika Uwanja wa Maonesho wa Mwl J.K Nyerere Dar es Salaam. Huduma zinazotolewa na BRELA katika Maonesho ni Usajili wa Makampuni, Usajili wa Majina ya Biashara, Usajili wa Alama za Biashara na Huduma, Utoaji wa Hataza, Utoaji wa Leseni za Biashara Kundi A, Utoaji wa Leseni za Viwanda na Huduma za baada ya Usajili na Kupata Leseni.
Posted by MROKI On Wednesday, July 07, 2021 No comments

October 19, 2020

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge,akizungumza kwenye Semina ya wastaafu iliyoandaliwa na benki ya CRDB kwa lengo la kuwajengea uwezo kwa kutunza na kuwekeza katika masuala mbalimbali yanayopatikana katika benki hiyo leo jijini Dodoma.

 

Baadhi ya washiriki wa mafunzo wakisikiliza hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge (hayupo pichani) wakati wa  Semina ya wastaafu iliyoandaliwa na benki ya CRDB kwa lengo la kuwajengea uwezo kwa kutunza na kuwekeza katika masuala mbalimbali yanayopatikana katika benki hiyo leo jijini Dodoma.

Meneja wa Benki ya CRDB Kada ya Kati Bi.Chabu Mishwaro,akitoa taarifa jinsi walivyobunifu wazo hilo kwa wastaafu katika semina ya wastaafu iliyoandaliwa na benki hiyo yenye lengo la kuwajengea uwezo kwa kutunza na kuwekeza katika masuala mbalimbali yanayopatikana katika benki hiyo leo jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Semina ya wastaafu iliyoandaliwa na benki ya CRDB kwa lengo la kuwajengea uwezo kwa kutunza na kuwekeza katika masuala mbalimbali yanayopatikana katika benki hiyo leo jijini Dodoma.

**************

Na Mwandishi wetu,Dodoma

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge amesema adhma ya serikali ni kuhakikisha inatengeneza maisha bora kwa wastaafu wote nchini kwa kuwajengea mazingira endelevu ya kujiingizia kipato

Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dodoma wakati wa mafunzo maalumu yaliyoandaliwa na benki ya CRDB kwa wastaafu hao yenye lengo ya kutoa fursa zinazopatikana hivyo  serikali imeaandaa mikakati kwa kushirikiana na benki hiyo ili kutoa fursa zitakazo wawezesha wastaafu nchini kuanzisha miradi yenye tija .

 ''Naipongoeza CRDB kwa kuendelea kuwa wabunifu kwa kuja na wazo hili la kuwakutanisha wastaafu ili kujadili kwa pamoja fursa zinazopatikana katika benki hii ukizingatia kundi hili la wateja limekuwa likisahaulika''amesema Dkt.Mahenge

 Aidha amesema kuwa CRDB imefanya jambo kubwa kwa kufanya semina kwa wastaafu maana ni kitu kigeni kwa benki ya mikopo kuwakutanisha wastaafu kwa kujadili pamoja na kuwapa mbinu na ujuzi kwa kunijiendeleza kimaendeleo kwa kuongeza kipato.

Dkt.Mahenge amewapongeza wastaafu wote walioitikia wito kwa kuja kujifunza mafunzo masula ya kibenki zitolewazo na CRDB imani yangu baada ya kongamano hili kutakuwa na mabadiliko makubwa katika utunzaji na uwekaji wa fedha pamoja na masuala ya mikopo.

''Leo ni siku muhimu kwa CRDB kwa kutukusanya hapa hivyo naamini baada ya mafunzo hayo tutapata elimu jinsi ya kuwekeza na kutunza masuala ya mikopo katika kuboresha maisha yetu''amesema Dkt.Mahenge

Hivyo niipongeza CRDB kwa kuanzisha na kutekeleza mpango huu wa uwezeshaji kwa wastaafu wenye lengo la kuleta faraja na kuwasaidia wastaafu katika kukidhi mahitaji yao mbalimbali ya kimaisha zote tumekuwa tukiona changamoto hivyo mpango huu utaleta tumaini jipya.

Kwa upande wake Meneja wa Benki ya CRDB Kada ya Kati Bi.Chabu Mishwaro,amesema kuwa CRDB ni bunifu ni benki ambayo inasikiliza mahitaji yote ya Mtanzania kwenye familia yake tunajua tunatengemeana sana katika kusikilizana masuala mazima na mahitaji kwa wateja wetu.

''Hivyo benki yetu tumeamua kubuni ubunifu kwa wastaafu kwa kuwaleta hapa leo na kuwafunza namna ya kuwajengea uwezo pamoja fursa mbalimbali zilizopo katika benki yetu na jinsi ya kutumia mikopo pindi wanavyostaafu wajione kama bado wapo kazini''amesema Bi.Mishwaro

Posted by MROKI On Monday, October 19, 2020 No comments

October 13, 2019

 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Mary Maganga, akizungumza jambo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Hazina Saccos leo jijini Dar es Salaam,ambapo amekipongeza chama hicho kwa kuwapatia viwanja wanachama wake na kuwataka waliopata viwanja hivyo waviendeleze. 

 Mwenyekiti wa Bodi wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Hazina Saccos,Bw. Aliko Mwaiteleke akifafanua jambo mbele ya Wanachama  waliohudhuria mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama hicho uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano Hazina, leo jijini Dar es Salaam. 
  Meneja wa Hazina Saccos Bw. Festo Mwaipaja akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya majukumu ya Saccos hiyo kwa wajumbe wa mkutano Mkuu wa mwaka wa chama hicho jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Hazina Saccos wakifuatilia yaliyokuwa yakijadiliwa wakati wa Mkutano huo uliofunguliwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Mary Maganga (hayupo pichani). 
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Mary Maganga wa nne kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Sekretarieti ya bodi ya Hazina Saccos baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Chama hicho cha Ushirika jijini Dar es Salaam.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango).
 ************ 

Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam
CHAMA cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Hazina Saccos kimeazimia kujenga kitega uchumi cha kisasa kwa gharamaya  Shilingi bilioni 52 kupitia mradi wa Njedengwa katika Jiji la Dodoma ili kukuza uchumi wa mkoa wa Dodoma na Taifa kwa kupitia kodi.
Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi wa chama hicho cha Ushirika Bw. Aliko Mwaiteleke  wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka  uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano Hazina,  na kuongeza kuwa mradi huo upo katika hatua za mwisho za utekelezaji wake.
Mwaiteleke alisema mpaka sasa upembuzi yakinifu wa mradi huo utakaojengwa kwa njia ya ubia kati ya Hazina Saccos na mwekezaji kwenye neo lenye ukubwa wa ekari 22  kupitia utaratibu wa Jenga, Endesha na Hamisha (Build, Operate and Transfer - BOT) ambapo mwekezaji atagharamia ujenzi wote na kuendesha kwa muda ambao utakubaliwa ndani ya mkataba.
Alisema mradi huo unasimamiwa na Kamati ya watu Saba wakiongozwa na Profesa Esta Eshengoma kutoka Chuo Kiuu Cha Dar es Salaam na wajumbe wake kutoka Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru),  Bodi ya Manunuzi ya Umma (PSPTB), Kituo Cha Uwekezaji (TIC), na Chuo Kikuu cha Ardhi ambao kwa sasa wanafanya kazi ya kusaka mwekezaji ili kufanikisha mradi huo.
Bw. Mwaiteleke alifafanua kuwa Mradi wa Njedengwa upo mbioni kuanza  na unategemewa kuwa chachu ya maendeleo ya chama hicho kwa kukiingizia kipato kutokana na shughuli zitakazokuwa zikifanyika kupitia mradi huo.
Alifafanua kuwa  mradi huo utahusisha ujenzi wa hoteli ya kisasa, kumbi za  mikutano, majengo ya Ofisi,  Viwanja vya Michezo na bwawa maalum la kuogelea.
Aidha alisema Chama hicho cha Hazina Saccos ambacho kina wanachama 5,600 kina mtaji mtaji wenye thamani ya shilingi bilioni 10 ikiwa ni fedha taslimu na mali wanazozimiliki ikiwemo ardhi ambazo zimekuwa na manufaa makubwa kwa wanachama..
"Mwaka jana pekee kupitia akiba na mikopo  tulipata faida ya shilingi milioni 64 na kila mwanachama alipewa gawio la asilimia 20 kulingana na hisa zake"alisema Mwaiteleke.
Alisema faida nyingine waliyopata kupitia Hazina Saccoss ni kununua viwanja 150 katika maeneo mbali mbali ya mkoa wa Dar es Salaam na Pwani na kuwakopesha wanachama wao kwa bei nafuu ambapo wanalipa kidogo kidogo kwa miezi 60.
"Pia Dodoma tumenunua viwanja 897 katika maeneo ya Ihumwa Ngaloni, Iyumbu  (maeneo ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambavyo tumevigawa kwa wananchi na viwanja vya Nzuguni tutaanza kuvigawa baada ya taratibu za Halmashauri ya Jiji la Dodoma kukamilika ili kuwawezesha wanachama wetu waliohamia Dodoma kupata maeneo ya kujenga makazi yao” alisema Bw. Mwaiteleke
Naye Meneja wa Hazina Saccos Bw. Festo Mwaipaja, alisema Saccoss hiyo sio ya wafanyakazi wa Wizara ya Fedha peke yake bali watumishi wote wa serikali wanaruhusiwa kujiunga na chama hicho isipokua vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo ni jeshi, Polisi, na Usalama wa  Taifa.
Alisema kwa mtumishi wa umma kujiunga na chama hicho cha ushirika mbali na kuwa muajiriwa pia atapaswa kulipa kingilio cha shilingi 20,000 na kununua hisa kuanzia 20 ambazo kila hisa moja ni shilingi 10,000 na kufanya thamani ya hisa zote kuwa shilingi 200,000.
Aidha alisema kuna mchango wa shilingi 20,000 kila mwezi na kuwataka watumishi wa umma kutoka taasisi na idara zote za serikali kuchangamkia fursa ya kujiunga na ushirika huo ili kujiinua kiuchumi
Kuhusu viwanja, Bw. Mwaipaja alieleza kuwa Chama hicho kimetumia zaidi ya shilingi bilioni 4 kununua viwanja katika Jiji la Dodoma na kuchangia eneo hilo kuwa na mzunguko mkubwa wa fedha kwa wenyeji na kwamba hayo ni mafanikio yanayoihusu jamii.
Akifungua Mkutano Mkuu huo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Mary Maganga, ameipongeza Hazina Saccos kwa kuwapatia viwanja wanachama wake na kuwataka wanachama waliopata fursa ya kupata viwanja hivyo waviendeleze haraka ili kuodokana na changamoto ya malazi kwa kuwa baadhi walipata viwanja hivyo tangu mwaka uliopita, 2018.
Aidha, ameipata kongole Hazina Saccos kwa hatua waliyofikia ya kutafuta mwekezaji katika mradi wa Njedengwa ambao utaongeza mapato ya Ushirika na kuwataka viongozi na wanachama kuhakikisha wanazingatia taratibu Sheria na Kanuni ili kufanikisha mradi huo muhimu.
Posted by MROKI On Sunday, October 13, 2019 No comments
  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo