WANASAYANSI wanasema kuwa
majaribio ya awali yanaonyesha kuwa siku za usoni itawezekana kuwatengeneza
watoto bila ya kutumia mayai ya mama.
Wanasayansi hao wamefaulu kutengeneza watoto wa panya kwa
kutumia mbegu za kiume na kuziunganisha na seli za kawaida kwa kuzidanganya
kudhani kwamba zitatungisha mayai ya kawaida ya uzazi wa panya hao.
Uchunguzi huu unamaanisha kuwa siku za usoni huenda wanawake
wasishirikishwe katika utengenezaji wa watoto kabisa, watafiti wanasema kwenye
matokeo ya utafiti huo ambayo yamechapishwa kwenye jarida la kimatibabu la
Nature Communications.
Wanasayansi hao kutoka Chuo Kikuu cha Bath walianza majaribio
hayo kwa kutumia mayai ya uzazi ambayo hayajatungishwa mbegu za kiume.
Walitumia kemikali kufanya ujanja fulani ambao ulielekeza
mayai hayo ya uzazi kuwa makamilifu.
Mayai haya ya bandia yanafanana au yana sifa nyingi zilizo
sawa sana seli za kawaida kama vile seli za ngozi, katika njia ambayo
zinajigawanya na pia kudhibiti chembe zinazoamua maumbile ya viumbe au DNA.
Watafiti wanasema kuwa iwapo kwa kutungisha mbegu za kiume
kwenye mayai bandia kunaweza kuzalisha watoto wenye afya kwa panya, basi
inamaanisha kuwa siku za usoni mpango huo unaweza ukatumiwa kwa mwanadamu na
kwa kutumia seli ambazo ambazo hazitoki kwenye mayai ya uzazi.
Katika majaribio ya panya, uwezekano wa upachikaji mimba
uliweza kufaulu mara moja kwa kila mara nne. Hii ni sawa na asilimia 25.
Dkt Tony Perry, mmoja wa watafiti hao aliambia BBC kuwa:
"Hi ni mara ya kwanza kwa mtu yeyote kuweza kuthibitisha kwamba kitu
kingine chochote, isipokuwa mayai ya uzazi, kinaweza kuungana na mbegu za kiume
ili kuzalisha mtoto. Hali hii inafutilia mbali dhana ambayo imekuwepo kwa zaidi
ya miaka 200." ISOME ZAIDI HAPA BBC
0 comments:
Post a Comment