Wachezaji wa timu ya netiboli ya Uchukuzi SC
wakifanya mazoezi ya viungo kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Wachezaji wa timu ya netiboli ya Uchukuzi SC
wakisikiliza maelekezo ya kocha Judith Ilunda (mwenye tisheti nyeupe
anayetazama kamera
Mchezaji Subira Jumanne wa Uchukuzi SC akiwahi mpira.
****************
TIMU ya Uchukuzi SC imesema
haina wachezaji mamluki watakaowatumia katika mashindano ya Mei Mosi
yatakayoanza Jumatatu (Aprili 18), kwenye viwanja vya Jamhuri mkoani Dodoma.
Mwenyekiti wa Uchukuzi SC,
Mohamed Ally, alisema jijini hapa kuwa hawawezi kutumia mamluki kwani ni moja
ya masharti na kanuni ya mashindano hayo, kwani hairuhusiwi kutumia wachezaji
ambao sio waajiriwa wa taasisi au wizara zinazoshiriki kwenye mashindano hayo.
“Tumekuwa tukishiri haya
mashindano na mengine mengi yanayoshirikisha taasisi za serikali na moja ya
masharti makubwa ni kutotumia wachezaji wasiokuwa wafanyakazi halisi
wanatambulika kama mamluki, hili tulisimamia kwa kuhakikisha wafanyakazi
waajiriwa katika idara mbalimbali ndio wanaocheza katika mashindano haya”
alisema Ally. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Ally alisema wanawachezaji
wengi wenye viwango vya juu, ambao wanauhakika wa kufanya vizuri kwa kuchukua
ubingwa katika michezo mbalimbali baada ya kufanya mazoezi kwa muda mrefu.
“Tuliweka kambi kwa takribani
miezi miwili huku tukifanya mazoezi kwenye viwanja vyetu vilivyopo kando kando
ya uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na baadaye tukacheza mechi za
kirafiki na timu mbalimbali za soka ikiwemo Amadori Boys ya Pugu Sekondari,”
alisema Ally.
Naye kocha wa timu ya netiboli
ya Uchukuzi SC, Judith Ilunda alisema hana hofu na wachezaji wake kutokana kufanya
mazoezi ya kutosha kwa kucheza mechi tatu za kitafiki na timu za Uhamiaji na Cargo.
“Tunauhakika wa kutwaa kombe
kwa sababu tumefanya maandalizi kabambe na tuna wachezaji wazoefu, wakiwemo
waliowahi kuchezea timu ya taifa na wengine bado wapo katika timu hiyo ya
taifa,” alisema Ilunda mchezaji wa zamani wa timu machachari ya Bandari na timu
ya taifa.
Aliwataja baadhi ya wachezaji
hao wazoefu ni pamoja na Matalena Mhagama, Mwadawa Hamisi, Subira Jumanne, Mary
Kajigili na Sharifa Mustafa.
Meneja na kocha wa timu ya
soka ya Uchukuzi SC, Robert Damiani alisema wapo tayari kwa mashindano kutokana
na maandalizi kamambe waliyoyafanya wakiwa jijini Dar es Salaam.
Kocha wa timu ya riadha wa
Uchukuzi SC, Kingsley Marwilo alisema atakuwa wachezaji watatu wa marathoni,
ambao ni Scolastica Hasiri, Ramadhani Mwakilongo na Leonard Julius.
Timu ya Uchukuzi SC, ambayo
inashiriki kwenye michezo ya soka, netiboli, riadha, baiskeli, kuvuta kamba,
karata, bao na vishale, mwaka jana ilitwaa vikombe 13 kati ya hivyo vitano
vilikuwa vya ubingwa wa kwanza, na vilivyosalia vilikuwa vya ushindi wa pili na
tatu.
0 comments:
Post a Comment