WIZARA ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano inapenda kutaarifu Umma kuwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, anatarajiwa kuwa
mgeni rasmi katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa barabara
ya juu (Flyover) katika makutano ya
TAZARA na ufunguzi wa Daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Siku ya Jumamosi
tarehe 16 Aprili, 2016 Mheshimiwa Rais ataweka jiwe na msingi la ujenzi wa
barabara ya juu katika makutano ya barabara Nyerere na Mandela (Flyover ya TAZARA).
Jumanne
tarehe 19 Aprili, 2016 Mheshimiwa Rais atafungua rasmi Daraja la Kigamboni
lenye urefu wa mita 680 na barabara unganishi (approach roads) upande wa Kurasini na Kigamboni zenye urefu wa
kilometa 2.5. Ujenzi huu umefanywa na
Kampuni ya China Railway 15 Group ilishirikiana na Kampuni ya China Bridge
Engineering Group.
Aidha wakati
tunasubiri uzinduzi rasmi, Wananchi na magari yenye uzito usiozidi tani 10
yataruhusiwa kutumia Daraja la Kigamboni kuanzia Jumamosi tarehe 16 Aprili,
2016 ili kuwawezesha kuelewa vizuri miundombinu na matumizi ya daraja.
Utekelezaji
wa miradi hii ni mojawapo ya jitihada za Serikali za kuboresha miundomninu na
kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment