Muinekano wa juu wa Daraja la ksiasa la Kigamboni na njia ambazo zitatumika kuingilia darajani humo kwa upande wa Kurasini. Daraja hilo linalounganisha eneo la Kigamboni na upande wa Kurasini likikatisha bahari ya Hindi. Rais Dkt. John Pombe Magufuli analizindua tarajiwa kulizindua rasmi daraja hilo Jumanne Aprili 19, 2016.
NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said, Kurasini
ZAMANI kwa mgeni aingiae jiji la
Dar es Salaam, ataambiwa “Kashangae Ferry” lakini mgeni atakayeingia leo
jijini, ataambiwa Kashangae Kurasini-daraja la Kigamboni.
Hiyo ndiyo hali halisi ilivyokwa
sasa ambapo mamia yawakazi wa jiji wamekuwa wakienda kwenye Daraja la kisasa la
Kigamboni mosi kushangaa maajabu ya daraja lenyewe ambalo ni refu kuliko
madaraja yote hapa nchini pengine Afrika Mashariki, lakini pili kupiga picha za
kisasa “Selfie”.
Daraja hilo lenye urefu wa mita 680
likiunganisha eneo la Kigamboni na Kurasini wilayani temeke jijini Dar es
Salaam. Kwa mujibu wa taarifa za wakandarasi wa mradi huo, Daraja hilo litakuwa
na barabara sita, tatu kila upande, na pia njia za waenda kwa miguu
(Pedestrians).
Hali pametengwa milango kwa ajili
ya matumizi ya magari aina tofauti.
Geti namba 1 ni kwa wale wenye
vibali maalum, geti namba 2 geti namba 3 na geti namba 4 ni wenye magari madogo
binafsi, geti namba 5 ni mini bus (daladala) na Geti namba 6 nimaalum kwa malori.
Daraja hilo ambalo ujenzi wake
umeanza Februari 1, 2012 ni mradi wa ubia kati ya Serikali yenye asilimia 40
naMfuko wa Hifadhi ya Jamii, NSSF yenye asilimia 60.
Daraja hilolinaongeza vivutio vikuu
viwili ambavyo wilayaya Temeke jijini Dar es Salaam inavyo, daraja lenyewe la
Kigamboni lakini pia uwanja wa kisasa wa taifa.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli
anatarajiwa kulizindua rasmi daraja hilo umanne Aprili 19, 2016 na tayari
maandalizi ya hafla hiyo yanaendelea ambapo K-VIAS MEDIA, imezuru eneo hilo leo
Aprili 18, 2016 na kujionea wajkandarasi namaafisa wa serikali wakiweka mambo
sawa tayari kwa shughuli hiyo muhimu katika historia ya nchi hii.
Lakini pia ukitaka kuona mfano wa “Flyover”
basi pitia hapo Kurasini uone jinsi barabar zilivyobebana kuelekea eneo la
daraja na zile zinazoungana na barabara ya Mandela.
Akina mama hawa na watoto wao walikuwa ni miongoni mwa wakazi wa jiji la Dar es Salaamwanaofika kulishangaa daraja hilo la kisasa
Barabara inayoelekea kwenye daraja hilo
0 comments:
Post a Comment