Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akisalimiana na
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa
Nchi kavu na Majini (SUMATRA), Bw. Gilliard Ngewe,wakati alipotembelea Ofisi za
Mamlaka hiyo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Nchi kavu
na Majini (SUMATRA), Bw. Gilliard Ngewe akitoa ufafanuzi wa shughuli
zinazofanywa na Mamlaka hiyo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa wakati alipotembelea Ofisi za Mamlaka hiyo.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa
Menejimenti ya Mamlaka ya Usafiri wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA), Bw.
Gilliard Ngewe, wakati alipotembelea Ofisi za Mamlaka hiyo.
Watumishi
wa Mamlaka ya Usafiri wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA), wakimsikiliza Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa(hayupo pichani), wakati
alipokutana nao.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa
wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa
Nchi kavu na Majini (SUMATRA), alipokutana nao. SOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiagana na watumishi
wa Mamlaka ya Usafiri wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA) mara baada ya kukutana
nao.
****************
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka Mamlaka ya Usafiri wa
Nchi kavu na Majini (SUMATRA), kudhibiti wasafirishaji wasio waaminifu, wanaobadilisha
ruti za safari na kuongeza nauli nyakati za asubuhi na jioni nchini.
Akizungumza na
wafanyakazi wa SUMATRA amewataka kutengeneza mkakati utakaoboresha huduma za
usafiri na kupunguza ajali za barabarani
nchini kote.
“Sumatra mna mchango
mkubwa wa kusimamia sekta ya usafirishaji nchini, hatutaki kuona nauli
zinabadilika nyakati za asubuhi na jioni na kusababisha usumbufu kwa abiria”,
amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Amewataka SUMATRA
kutosita kuchukua sheria kwa yeyote anayekiuka taratibu za usafiri, kujenga
mazingira sawia ya ushindani, kusimamia gharama na viwango vya huduma na kutoa
leseni kwa wasafirishaji kwa haraka.
Waziri Prof. Mbarawa
ameipongeza Mamlaka kwa jitihada wanazozifanya za kuweka mifumo ya utendaji wa
kieletroniki itakayo ratibu mabasi yawapo safarini ili kupunguza mwendo kasi na
kupunguza ajali.
Aidha Waziri Mbarawa
ameitaka SUMATRA kukusanya mapato yanayostahili kikamilifu na kupunguza
matumizi yasiyo ya lazima.
Kwa upande mwingine Waziri
Mbarawa ameitaka Mamlaka hiyo kusimamia mfumo uliopo wa kieletroniki kwa ajili
ya kupata leseni kwa muda usiozidi miezi miwili.
Mkurugenzi Mkuu wa
SUMATRA Bw. Giliard Ngewe amemhakikishia Waziri Mbarawa kuwa Mamlaka inaendelea
kutoa elimu kwa madereva kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kupunguza
ajali za barabarani na kuboresha huduma za usafiri nchini.
“Tumejipanga
kuhakikisha maeneo yenye upungufu wa mabasi ya abiria yanapatiwa ruti mpya ili
kupunguza changamoto katika maeneo
ambayo yana changamoto ya usafiri”, amefafanua Waziri Mbarawa
Katika hatua nyingine
Prof. Mbarawa ameitaka SUMATRA kuangalia namna ya kutenganisha udhibiti wa
usafiri wa majini na Nchi kavu ili kuongeza tija na kukuza sekta hizo hapa
nchini.
“Kukiwa na udhibiti wa
usafiri wa majini (Maritime Authority) kutasaidia kukuza sekta hiyo na Sumatra
kuendelea kudhibiti usafiri wa nchi kavu (reli na barabara)”, amesisitiza
Waziri Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa alikuwa
katika ziara ya kikazi ya kutoa miongozo na muelekeo wa serikali ya Awamu ya
Tano ambapo amesisitiza uadilifu, uwazi, na utendaji kazi wenye malengo yanayopimika,
Katika mikakati ya
kudhibiti usafiri wa nchi kavu SUMATRA imepanga kuunganisha mikoa yote 25 ya
Tanzania Bara kwenye mfumo wa kompyuta ili kutoa leseni kwa haraka na kuongeza
mapato ambapo takribani shilingi bilioni 45 zinatarajiwa kukusanywa katika
mwaka huu wa fedha.
0 comments:
Post a Comment