Golikipa mahili wa Mbeya City
Fc, Juma K Juma amerejea kikosini kutoa mapumziko ya majuma mawili
aliyopewa na kocha Kinnah Phiri kufuatia mkewe Bi Nasra Nassor
kujifungua watoto mapacha hivi karibuni.
Akizungumza na mbeyacityfc.com
muda mfupi uliopita Kaseja amesema kuwa amefurahi kusafiri na hatimaye
kurudi salama kwenye timu yake huku pia akitoa shukurani zake za dhati wa wale
wote ambao wamekuwa karibu nae yeye kama mchezaji na pia familia yake tangu
alipojiunga na City.
“Nashukuru mungu nimefika hapa salama baada ya
safari yangu, pia namshukuru kwa kile alichonijaalia, nimerudi kikosini nikiwa
na ari kubwa zaidi ili kuituikia timu yangu kwa nguvu zote katika
kutafuta mafanikio hasa kwenye kipindi hiki ambacho ligi inaelekea
mwishoni, hakika tunapita kwenye kipindi kigumu lakini umoja wetu
utatufanya kuvuka hapa” alisema.
Akiendelea zaidi Kaseja
aliyewahi kucheza kwa mafanikio kwenye timu za Moro United, Simba, na
Yanga aliweka wazi kuwa anaimani kuwa na kocha Kinnah Phiri kuwa ataijenga upya
City na kuifanya kuwa timu itakayotisha zaidi kwenye msimu ujao wa ligi kuu ya
Vodacom Tanzania Bara.
0 comments:
Post a Comment