NA K-VIS MEDIA Na Mashirikaya
Habari
HILARY Clincton, (Pichani
juu), ambaye anaomba kuteuliwa na chama chake cha Democrat, kuwania kiti
charais wa Marekani kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika nchini humo, ameshindwa
kwenye mchujo wa uteuzi katika jimbo na New Hamshire.
Pia Mgombea wa chama cha
Republican, Donald Trump, ameshinda kwenye mchujo wa uteuzi katika jimbo
hilo la New Hamshire uliofanyika Jumanne usiku.
Seneta wa Vermont Bernie
Sanders, ndiye aliyemshinda Hillary Clinton, huku Trump, tajiri mkubwa
kutokaNew York, na ambaye amekuwa akiwashutumu wageni hususan Waislamu kuwa
wanaleta “shobo” nchini humo yeye amewabwaga mahasimu wake wa karibu Gavana wa
Ohio, John Kasich aliyeshika nafasi ya pili, Gavana wa Florida, Jeb Bush,
Seneta wa Texas, Ted Cruz na Seneta wa Florida, Marco Rubio.
Trump na Seneta Sanders wote
wawili wamekuwa wakiwataka watu wapige kura dhidi ya watu ambao tayari wamekuwa
kwenye mfumo wa utawala wa nchi hiyo.
Clinton ambaye aliwahi kuwa
Waziri wa Mamboya Nje wa Marekani kwenye utawala wa sasa wa Obama, tayari
amempongeza Bw Sanders, lakini akasema ataendelea kupigania kila kura kwenye
kinyang’anyiro hicho cha kumtafuta mgombea urais wa chama cha Democratic.
Seneta Bernie Sanders (kushoto) na Tajiri Donald Trump.
0 comments:
Post a Comment