Timu ya Taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’ inayonolewa na kocha mkuu
Rogasian Kaijage imendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo wa kirafiki
dhidi ya Timu ya Taifa ya Wanawake ya Malawi utakaochezwa Novemba 07,
mwaka huu jijini Dar es salaam katika uwanja wa Azam Chamazi.
Twiga Stars iliingia kambini Oktoba 29, katika hosteli za Shirikisho
zilizopo Karume, ina kikosi cha wachezaji 22 wanaofanya mazoezi asubuhi
na jioni katika uwanja wa Karume.
Mchezo dhidi ya Malawi ni mchezo wa kirafiki wa kimataifa, ambao
kocha Kaijage atautumia kuangalia maendeleo ya wachezaji wake kwa ajili
ya maandalizi ya micheo ya kimataifa.
Wachezaji waliopo kambini ni Asha Rashid, Estha Chaburuma, Fatuma
Bushiri, Fatuma Omari, Mwajuma Abdallah, Mwanahamis Omar, Fatuma
Khatibu, Amina Ally, Fatuma Issa, Belina Julius, Happines Hezron na
Donizia Daniel.
Wengine ni Maimuma Hamisi, Stumai Abdallah, Anna Hebron, Anastazia
Anthony, Shelder Boniface, Wema Richard, Tumaini Michael, Jane Cloudy,
Saada Ramadhani na Sofia Mwasikili.
0 comments:
Post a Comment