Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa Kampuni ya Total
Tanzania,Marsha Kilewo, akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa
kutangaza kuzinduliwa kwa shindano la “Startupper of the year by Total” ambalo litashirikisha vijana wenye
mawazo ya kibiashara na kuweza kushinda hadi sh milioni 35.
KAMPUNI
ya Total ya Tanzania, yazindua Shindano
la Total «Startupper of the year by Total», lililobuniwa na kundi la Makampuni
ya Total litakaloshirikisha nchi 34 za Afrika kwa wakati mmoja. Shindano hilo linalenga katika kutambua, kuzawadia na
kuwezesha utekelezaji wa miradi bora ya biashara ya ujasiliamali inayoanza au
iliyobuniwa chini ya miaka miwili kwa ajili ya maendeleo ya jamii na taifa.
Washindi
wa miradi bora watapewa tuzo ya « Startupper of the year 2016 by Total »
itakayoambatana na fedha taslimu
itakayotumika kama mtaji wa kuendeleza, na kusimamia uendeshaji wa miradi hiyo.
Shidano
hili ni bure kwa raia wote wa Watanzania
wenye umri kati ya miaka kumi na nane( (18) hadi miaka thelathini na tano (35).
Fomu
za maombi zimeanza kutolewa kuanzia tarehe 1 Novemba 2015 saa 2:00 asubuhi
kwenye tovuti: http://startupper.total.com/.
Shindano litakuwa wazi hadi Januari 31, 2016 saa 5:00 asubuhi ambapo
ndio mwisho wa kurejesha fomu.
Jopo
la Majaji linalohusisha wataalamu wa
biashara, litachagua miradi kumi bora
nchini Tanzania itakayoingia fainali kwa kuzingatia vigezo vya ubunifu,
uhalisia na uwezo wa mradi katika kuleta maendeleo na kuboresha hali ya maisha
ya jamii kubwa ya Watanzania.
Orodha
ya washindi watakaoingia fainali itachapishwa tarehe 28, Februari, 2016 katika
tovuti ile ile walipochukulia fomu za kugombea.
Kuanzia
tarehe 15 Machi, 2016, Washindi hao kumi, wataingia katika mchuano wa
fainali kutafuta tatu bora ambapo
washindi watawajibika kuitetea miradi yao
mbele ya jopo la majaji ili kupata miradi mitatu bora ambapo mshindi wa jumla atatangazwa na kupewa
zawadi katika hafla maalum ya utoaji wa tuzo.
Sheria, taratibu, kanuni na vigezo vya
shindano hili zinapatikana bure kwenye
tovuti ya (http://startupper.total.com/).
Shindano
la « Startupper of the year by Total » ni juhudi za Kampuni ya kimataifa ya
Total katika kuhamasisha maendeleo ya
kiuchumi na kijamii ili kusaidia nchi
zote duniani ambako kampuni ya Total
ipo. Shindano hili ni hatua madhubuti yenye lengo la kuvumbua ubunifu wa miradi mbalimbali ya maendeleo yenye lengo la
kuchangia uanzishwaji wa viwanda vidogo vitakavyotoa ajira na kuchangia
maendeleo ya jamii na ya nchi za bara la Afrika kwa ujumla.
Shindano
hili linalenga kuibua miradi mipya, iliyotokana na wananchi wenyewe ambayo
inaendana na malengo ya jumla ya uwepo wa kampuni ya Total.
0 comments:
Post a Comment