Mkurugenzi Mstaafu wa Idara ya
Misitu na Nyuki, Dk. Felician Kilahama, akiwasilisha mada juu ya utafiti alioufanya maeneo mbalimbali nchini juu ya uhifadhi misitu.
Washiriki wa semina hiyo ya siku moja wakifuatilia mada mbalimbali katika seimina hiyo Dar es Salaam jana.
***************
SERIKALI imetakiwa kuongeza nguvu katika uhifadhi
na usimimamizi wa misutu nchini, ili kuendana na kasi ya matumizi ya Bidhaa za
misutu kwa taifa.
Mkurugenzi Mstaafu wa Idara ya
Misitu na Nyuki, Dk. Felician Kilahama, alisema hali ya misutu ni mbaya na ipo
haja ya serikali kuongeza nguvu katika utunzaji wa misutu hiyo kama inavyo
fanya katika uhimizaji wa ukusanyaji mapato ya bidhaa za msitu.
“Misitu mingi iliyopo nchini, haina
mpangio wa usimamizi nchini ambao
unaainisha ni bidhaa gani itavunwa wapi na kwa kipindi gani huku pakiwa na
muelekeo unao onyesha makusanyanyo kutokana na usimamizi huo,”alisema Dk
Kilahama. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Kilahama alisema misitu inafaida
nyingi tofauti na inavyoonekana hivi sasa ya faida upande wa uvunaji magogo na
uchomaji mkaa ambao huingiza fedha kwa njia ya ushuru na faini mbalimbali
lakini misitu ndio chanzo cha mvua na upatikanaji wa maji na pia kukabiliana na
hewa ukaa ambayo nitishio kwa sasa.
Aidha amesema kuwa lengo kuu la
serikali kuanzisha wakala wa misitu nchini ni pamoja na kusimamia misitu ambayo
ikisimamiwa vizuri italeta faida kubwa zaidi kuliko ukusanyaji fedha.
Mapema akizungumza wakati wa
ufunguzi wa semina hiyo Mkurugenzi wa
Shirika la AWF na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la kuhifadhi Misititu ya Asili
Tanzania (TFCG),John Salehe alisema kuwa watanzania hivi sasa wanatakiwa wawe
mstari wa mbele katika utunzaji wa misitu nchini na si kuiachia serikali pekee.
Salehe amesema ipo haja ya viongozi
wa dini mbalimbali nchini wakatumiwa muda wao katika mahubiri yao kuelimisha
waumini wao juu ya umuhimu wa utunzaji misitu.
“Misitu ya hifadhi ipo maeneo mengi
nchini na miongoni mwa hiyo inazunguka katika vijiji vyetu, hivyo ipo haja ya
viongozi wa dini kushirikiana na mamlaka husika kutoa elimu ya uhifadhi misitu
katika kukabiliana na mabidiliko ya tabia nchi,”alisema Saleme.
Nae Afisa Misitu Mkuu wa Wakala wa
Huduma za Misitu na Mratibu wa Misitu
Asilia na mazingira asilia Tanzania, mradi, Gerald Kamwenda amesema wananchi
wanatakiwa kubadili mtindo wao wa maisha ili kuokoa misitu nchini.
Tanzania inakabiliwa na matatizo ya
tabia nchi lakini bado wananchi wanaendelea na uharibifu wa misitu hasa
matumizi ya mkaa na kilimo cha kuhamahama.
“Tumegundua gesi ya kutosha hivyo
wananchi wabadili matumizi kutoka kwenye mkaa hasa mijini na kutumia nishati ya
gesi na umeme, vijijini wanachoma mkaa kwaajili ya kuiuza kwa watu wa
mjini,”alisema Kamwenda.
Washiriki wa semina hiyo ya siku moja wakifuatilia mada mbalimbali katika seimina hiyo Dar es Salaam jana.
0 comments:
Post a Comment