Nafasi Ya Matangazo

November 11, 2015

Mashindano ya Miss Universe Tanzania yameanza rasmi katika kumtafuta mrithi wa taji la  Miss Universe Tanzania 2015 toka kwa Caroline Bernard.
Mpaka sasa hivi waandaaji wameanza kupokea fomu na picha za warembo kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania na Zanzibar.

Miongoni mwa mikoa ambayo Miss Universe Tanzania imepokea na inaendelea kupokea fomu na picha za washiriki ni  Arusha, Mwanza, Tanga, Iringa, Mbeya na Dar es Salaam. Zoezi la usaili na kupokea fomu kutoka mikoani litahitimishwa siku ya Jumamos kwa kufanya usaili hapa Dar es salaam katika ukumbi wa King Solomon’s uliopo Kinondoni mkabala na Best Bite.

Warembo wote wenye sifa wanaombwa wajitokeze hata kama bado hawajachukua fomu kwani ukiondoa kugombania taji kubwa la Miss Universe Tanzania pia washindi wa pili na wa tatu hupata fursa ya kushiriki katika mashindano mengine madogo ikiwemo Miss Earth kwenda kushindana kimataifa kama wenzao waliotangulia.

Mashindano ya Miss Universe kwa hapa Tanzania yalianza rasmi mwaka 2007 ambapo Tanzania iliwakilishwa na Flaviana Matata na kufanikiwa kuingia katika kumi bora na mwaka 2008 yaliwakilishwa na Amanda Ole Sulul, mwaka 2009 Miss Universe Tanzania iliwakilishwa na Illuminata James,ambapo mwaka 2010 alikuwa ni Hellen Dausen, mwaka 2011 Nelly Kamwelu, mwaka 2012 Winfrida Dominic, mwaka 2013 Betty Omara ndiye aliyepeperusha bendera ya Tanzania na mwaka 2014 ni Caroline Bernard ambaye ndiye anayekabidhi taji mwaka huu.
Posted by MROKI On Wednesday, November 11, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo