Meneja
Uhusiano wa Kampuni ya Simu ya Mkononi ya Airtel Tanzania , Bi. Jane Matinde
akionyesha kadi mpya ya malipo inayotumia huduma ya Airtel Money iliyopewa jina
la Airtel Money ‘ Tap Tap’ katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kadi hiyo
uliofanyika mbagala nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana. Airtel inakuwa
kampuni ya kwanza ya simu nchini kuanzisha huduma kama hiyo ambapo mteja
anaweza uitumia kufanyia malipo
mbalimbali hata kama simu yake haipo hewani.
Meneja
Uhusiano wa Kampuni ya Simu ya Mkononi ya Airtel Tanzania , Bi. Jane Matinde
(wa pili kushoto) na Ofisa wa kitengo cha Airtel Money, Stephen Kimea, wakiwapa
baadhi ya wateja, Shabani Mneta (kulia) na Penina Mneta, kadi za Airtel
Money ‘Tap Tap’ mara baada ya kuunganishwa katika hafla ya uzinduzi
rasmi wa kadi hiyo ya malipo inayotumia huduma ya Aritel Money katika
kufanyia malipo mbalimbali. Uzinduzi huo ulifanyika mbagala zakhem nje kidogo
ya Jiji la Dar es Salaam jana. Airtel inakuwa kampuni ya kwanza ya simu nchini
kuanzisha huduma kama hiyo.
Ofisa
wa kitengo cha Airtel Money, Stephen Kimea (wa pili kulia) akielezea faida na
matumizi ya kadi ya malipo ya airtel money ‘Tap Tap’ katika hafla ya
uzinduzi rasmi wa kadi hiyo inayotumia huduma ya Aitel Money katika
kufanyia malipo mbalimbali. Uzinduzi huo ulifanyika mbagala zakhem nje kidogo
ya Jiji la Dar es Salaam jana. Airtel inakuwa kampuni ya kwanza ya simu nchini
kuanzisha huduma kama hiyo. Kulia ni Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo,
Jane Matinde (kulia).
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya kutoka kundi la Tip Top Connection, Hamadi Seneda
‘Madee’ akiimba katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kadi ya malipo ya airtel
money ‘Tap Tap’ inayotumia huduma ya Airtel Money katika kufanyia malipo
mbalimbali. Uzinduzi huo ulifanyika mbagala zakhem nje kidogo ya Jiji la Dar es
Salaam jana. Airtel inakuwa kampuni ya kwanza ya simu nchini kuanzisha huduma
kama hiyo.
Mkali
wa miondoko ya kizazi kipya, Emmanuel Simwinga '*Izzo Business*' akiimba moja
ya nyimbo zake zilizompatia umaarufu ya ‘naongea na rizwani’ katika hafla ya
uzinduzi rasmi wa kadi ya malipo ya QAirtel Money ‘Tap Tap’ inayotumia huduma
ya Airtel Money katika kufanyia malipo mbalimbali. Uzinduzi huo ulifanyika
mbagala zakhem nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana. Airtel inakuwa kampuni
ya kwanza ya simu nchini kuanzisha huduma kama hiyo.
***********
Airtel Tanzania leo imezindua
huduma ya kwanza , ya kipekee na kibunifu yenye technologia ya kisasa
ijulikanayo kama “Tap Tap” itakayomuwezesha mtumiaji wa huduma ya Airtel
Money kufanya malipo kwa njia rahisi na,salama kupitia kadi hiyo Huduma hii itawewazesha wateja na jamii kwa ujumla kutumia maendeleo ya
technologia kuleta urahisi katika kuendesha maisha yao.
“Tap Tap”itawawezesha wateja
wa Airtel Money kufanya miamala kwa haraka na urahisi kwa kugusisha kadi zao
ambazo zimeunganishwa na akaunti ya Airtel money wakati wowote wanapotaka
kulipia huduma mbalimbali.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde alisema” Leo kwa mara nyingine tena Airtel tunachua hatua thabiti katika kuboresha maisha ya mamilioni ya wateja wetu kupitia uzinduzi wa huduma hii ya Tap Tap.
Kadi hii ni rahisi kutumia,
ili kufanya malipo mteja atagusisha kadi yake kwenye kifaa cha muuzaji na moja
kwa moja kufanya malipo kwa kuweka namba yako ya siri, wateja wetu wataweza
kulipia huduma mbalimbali katika vituo vya mafuta , maduka ya dawa, baa,
saloni, maduka ya rejareja, wataweza kununua muda wa maongezi kwa
mawakala wa Airtel Money.
Kupitia kadi hii tunawawezesha
watanzania kuwa na usalama na pesa zao na kuondoa haja ya mteja kutembea na pesa wakati wote. vilevile Mteja atakapopoteza
au kuibiwa kadi hela zake zitakuwa bado ni salama” Aliongeza kwa kusema ,
huduma ya “Tap Tap” inadhihirisha dhamira yetu ya kuboresha matumizi ya huduma za kifedha kupitia simu za mkononi na kutengeneza
njia mpya ya kufanya malipo katika technologia ya simu za mkononi na
kuwaondolea wateja wetu athari zitakazowapata kwa kutembea na pesa nyingi
mfukoni “ Tunaamini technologia hii mpya katika huduma za kifedha
kupitia simu za mkononi italeta njia mbadala wa kufanya malipo na pia kusaidia katika kuendelea kukuza na kutanua huduma za kifedha nchini.”
“Ni matumaini yetu kuwa wakazi katika maeneo ya Mbagala, Temeke, Tandika, Ubungo ambapo huduma hii imezinduliwa kwaoleo watafurahia faida zinazotokana na huduma hii ikiwa ni pamoja na kuboresha maisha yao kupita technologia hii ya kisasa” aliongeza Matinde
0 comments:
Post a Comment