Nafasi Ya Matangazo

June 08, 2015

KAMISHNA wa Sensa ya Watu na Makazi 2012, Hajat Amina Mrisho Said ametangaza nia ya kugombea Ubunge katika jimbo la Kiteto mkoani Manyara katika uchaguzi mkuu utakao fanyika baade mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam leo huku akiwa ameambatana na mumewe wake Alhaj Abeid Omary Khamis, Hajat Amina amesema ameamua kujitosa katika mchakato huo kupitia Chama cha Mapinduzi.

Aidha amesema endapo CCM itampa ridhaa ya kugombea kiti hicho anawahakikishia wananchi wa Kiteto uwakilishi na utumishji utakaowapendeza. 

"nawaahidi wananchi wa jimbo la Kiteto utumishi na uwakilishi mzyri, kikubwa ninacho waomba ni ushirikiano wao wote bila ubaguzi wa aina yeyote katika usimamizi na utekelezaji wa ilani ya CCM, katika jimbo letu,"alisema Hajat Amina.

Hajat amina amevitaja vipaumbele vyake vitano kuwa ni pamoja na kufuatilia kwa ukaribu utekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi,Kuiomba Serikali kufanikisha ujenzi wa Chuo cha Veta jimboni, Kuhamasisha uendelezaji wa ufugaji wenye tija kwa kufuatilia serikali iweke miundombinu ya ufugaji katika maeneo ya wafugaji.

vipaumbele vingine ni kuhamasisha ujenzi wa soko la Kimataifa la mazao hasa mahindi ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya matumizi ya stakabadhi ya mazao ghalani na kuanzisha mfumo huo jimboni na mwisho ni kuwashirikisha wananchi wote katika kujiletea maendeleo kwenye maeneo yao.
Posted by MROKI On Monday, June 08, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo