Nafasi Ya Matangazo

February 17, 2015

Utoaji wa vitambulisho vya taifa unaendelea jijini Dar es Salaam ambapo  Father Kidevu Blog ilitembelea moja ya kituo cha kutolea vitambulisho hicho kilichopo Ilala Bungoni na kukuta umati wa watu ukisubiri kupatiwa vitambulisho vyao. Katika eneo hilo kuna mitaa mbalimbali wengi ikiwa ni kutoka maeneo ya Vingunguti, Buguruni hadi Ilala mchikichini. Watu wa Pugu na maenweo ya Gongo la Mboto na Vitongoji vyake pia wanaendelea kupatiwa vitambulisho hivyo.
 Wananchi wakisubiri kupatiwa vitambulisho vyao.
 Mama huyu tayari ameshapata kitambulisho chake.
Kutokana na foleni iliyopo wakazi hawa wameamua kukaa chini kusubiri watu wapungue. Licha ya zoezi hilo kuendelea lakini baadhi ya watu wamelalamikia utaratibu wake wa kuwaleta watu kutoka maeneo ya mbali na badala yake watu hao wangekuwa wakienda katika maeneo yale yale waliyoandikishiwa.
Posted by MROKI On Tuesday, February 17, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo