Timu za African Sports
ya Tanga na Mwadui FC ya Shinyanga zinatrajiwa kucheza mchezo wa fainali ya
kusaka Bingwa wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) siku ya jumapili katika Uwanja wa
Taifa jijini Dar es salaam.
African Sports waliibuka
washindi wa kwanza katika Kundi A, na Mwadui FC washindi wa kwanza Kundi B
watacheza mchezo huo wa fainali ambapo Bingwa atapewa zawadi ya Kombe na
medali, hali kadhalika kwa msindi wa pili.
Ligi Daraja la Kwanza (FDL)
ilimalizika mwishoni mwa wiki kwa timu nne kupanda Ligi Kuu kwa kila kundi
kutoa timu mbili, Kundi A ni African Sports na Majimaji FC, Kundi B ni timu za
Mwadui FC na Toto Africans.
Nazo timu za Green
Worriors na Villa Squad zimeteremka Daraja la pili baada ya kushika nafasi za
mwisho kwenye msimamo wa Ligi Daraja la Kwanza, Villa Squad kutoka Kundi A na
Green Warriors Kundi B.
TFF YAZIPONGEZA AFRICAN SPORTS, MWADUI, MAJIMAJI
NA TOTO
Rais wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu nchini – TFF Bw. Jamal Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa Wenyekiti
wa klabu ya African Sports (Tanga) , Majimaji (Ruvuma), Mwadui (Shinyanga) na Toto Africans ya Mwanza
kwa timu zao kupanda Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).
Katika salamu zake Bw.
Malinzi amesema vilabu hivyo vinapaswa kujipanga na kufanya maandalizi kwa
ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom 2015/2016, kwani VPL ni ngumu
kutokana na timu zote kuwa na ushindani mkubwa wa kutafuta matokeo mazuri
kuepeuka kushuka daraja.
Kwa niaba ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini -TFF, familia ya mpira na watanzania kwa
ujumla wanawapa pongezi timu za African Sports, Majimaji, Mwadui na Toto
Africans kwa kupanda Ligi Kuu ya Vodacom na kuwatakia maandalizi mema ya VPL
2015/2016.
0 comments:
Post a Comment