Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Biswalo Mganga (pichani
katikati) kuwa kurugenzi wa Mashitaka (DPP) nchini.
Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar Es Salaam,
leo, Jumatatu, Oktoba 6, 2014, na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Bwana Peter
Ilomo imesema kuwa uteuzi huo umeanza Ijumaa iliyopita,
Oktoba 3, mwaka huu, 2014.
Kabla ya uteuzi wake, Bwana Mganga
alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka na Wakili wa
Serikali Mfawidhi.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment