Waziri mkuu wa zamani na mbunge wa Monduli Mh Edward
Lowassa(kulia)akiwakaribisha mawaziri wa zamani wa Kenya William ole
Ntimama(tai nyekundu) na John Keen(kushoto) nyumbani kwake Monduli.
Wanasiasa hao wakongwe na wenye ushawishi mkubwa katika eneo la Maasai
Land nchini Kenya walimtembelea Mh Lowassa ambaye ni Laigwanan mkuu wa
wamasai wote Afrika mashariki, na kujadiliana naye masuala mbalimbali
lakini zaidi ni juu ya suala la ardhi ambalo limekuwa tatizo kubwa kwa
jamii ya wamasai.Wazee hao wanatarajiwa kuudhuria semina maalum katika
jimbo la Monduli wiki ijayo kuzungumzia tatizo la ardhi.Semina
iliyoandaliwa na Mh Lowassa itawashirikisha viongozi wote wa wilaya hiyo
pamoja na wakuu wa kimila.Akizungumzia suala la ardhi mzee John Keen
alisema mtu anayeuza ardhi anauza utajiri na kununua umasikini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment