Tamasha hilo litaongozwa na waimbaji wa Nyimbo
za Injili wakubwa kutoka Kenya, Sara K, na Cristina Shusho kutoka
Tanzania, huku likipambwa na Ambwene Mwasongwe, Baraka Maasa, Eng calros
Mkundi, Ester Bukuku, Matha Mwaipaja, Nesta sanga, Meth Chengula,
Matumaini, Eline Patrick bila kuwasahau waimbaji wengine kutoka Mkoani
Arusha pamoja na Kwaya Mbalimbali.
Lengo la
tamasha hilo la UPENDO KWA MAMA linalengo la kutoa Mitaji kwa zaidi ya
akina mama 50 wajasiriamali ili kuwaongezea uwezo wa kujiajiri, vilevile
utakuwa ni wakati mwafaka wa kuwashukuru wakinamama wote kwa upendo
waliyonao ukiambatana na kujitolea katika kusimamia Familia na malezi ya
watoto.
Studio ya Mkundi nakamati ya
maandalizi ya Tamasha la UPENDO KWA MAMA wanatoa nafasi kwa watanzania,
Taasisi na Mashirika yote ambayo yako tayari kuungana na Studio ya
Mkundi kwa Ufadhili wa hali na mali ili kufanikisha tamasha hili la
UPENDO KWA MAMA.(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog Arusha)
0 comments:
Post a Comment