Waziri
wa Fedha, Dk. William Augustao Mgimwa (63)
amefariki dunia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa
za kifo cha Waziri wa Fedha, Mheshimiwa William Mgimwa, aliyekuwa pia Mbunge wa
Jimbo la Kalenga (Mkoa wa Iringa) kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Rais Kikwete amesema kuwa taifa limempoteza
Waziri Mgimwa katika kipindi lilipokuwa linamhitaji zaidi kutokana na mchango
wake mkubwa ambao amekuwa akiutoa kupitia nafasi zake za Waziri wa Serikali na
mwakilishi wa wananchi wa Jimbo la Kalenga.
Kifo cha Mheshimiwa Mgimwa kimetangazwa mchana
wa leo, Jumatano, Januari Mosi, 2014, na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi
Ombeni Sefue kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika tangazo lake, Balozi Sefue amesema kuwa
Waziri Mgimwa ameaga dunia asubuhi ya leo saa 5:20 (Saa za Afrika ya Kati)
katika Hospitali ya Kloof Medi-Clinic , Pretoria, Afrika Kusini ambako amekuwa
amelazwa kwa muda sasa.
Balozi Sefue amesema kuwa maandalizi ya kuurudisha
nyumbani mwili wa Waziri Mgimwa yanafanywa na Serikali kwa kushirikiana na
familia yake na kuwa taarifa zaidi za suala hilo zitatolewa baadaye kwa
kadri zinavyopatikana na maandalizi yanavyoendelea.
Katika salamu zake kwa Waziri Mkuu Mheshimiwa
Mizengo Pinda na kwa familia ya Marehemu Mgimwa, Rais Kikwete amesema: “Sina maneno ya kutosha kuelezea mshtuko na
huzuni yangu kubwa kufuatia taarifa za kifo cha Mheshimiwa Mgimwa.
Binafsi nimemtembelea mara mbili kwenye
Hospitali alikokuwa amelazwa na mara ya mwisho hali yake ilikuwa imeimarika. Tulizungumza
kwa kiasi cha dakika 10 hivi akanielezea nia yake na tamaa yake ya kurejea nyumbani
kwa sababu hali yake ilikuwa nzuri.”
Ameongeza Mheshimiwa Rais Kikwete: “Sote tunajua
mchango wake katika Serikali. Sote tulitamani kuendelea kuwa naye, lakini haya
ni mapenzi ya Mungu.”
“Napenda kutoa pole nyingi na rambirambi zangu
za dhati kwa wana-familia wote kwa kuondokewa na mhimili wao. Naungana nanyi
katika kuomboleza msiba huo mkubwa. Napenda mjue kuwa msiba huu ni msiba wangu
pia. Machungu yenu ni majonzi yangu,” amesema Rais Kikwete.
Rais pia amewatumia rambirambi wananchi wa Jimbo
la Kalenga akisema kuwa wamempoteza mwakilishi na mtetezi mahiri wa maslahi
yao.
Mgimwa aliyezaliwa January 20, 1950 na
kuwa mbunge wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa kupitia chama cha Mapinduzi (CCM)
mungu ailaze roho ya malehem mahali pema pepon amina bwana aliweka pia bwana ametwa jina lake lihimidiwe
ReplyDeleteBwana alitoa na ametwaa jina lake libarikiwe
ReplyDeleteBwana alitoa na Bwana ametwaa jina la bwana libarikiwe
ReplyDelete