2.
Mimi binafsi nitapata heshima ya kushiriki
kama kiongozi wa sekta binafsi chini ya TPSF. Lakini limekuwepo tatizo la mambo
yaliosemwa na Mhe. Profesa Muhongo kunihusu ambayo ningependa niyafafanue ili
nisiende kwenye kikao cha kesho zikiwepo fikra kwamba mambo hayo ni ya kweli.
3. Katika tarehe za mwanzo wa mwezi Septemba mwaka 2013 Mhe.
Profesa Muhongo alinukuliwa akisema kwamba:
“Mengi hana uzawa bali ubinafsi. Anataka kufanya udalali wa
vitalu vya raslimali zetu. Waelezeni Watanzania ukweli huu.”
|
|||
4. Ukweli ni kwamba mimi siyo mbinafsi na pili sijawahi
kuomba upendeleo wa kupewa kitalu cha gesi bali ninapigania Watanzania kwa
ujumla.
5. Tarehe 8 Desemba 2013, alipokuwa anajibu swali la Mhe.
Tundu Lissu kuhusu ni nani anamiliki migodi ya Tanzania, Mhe. Profesa Muhongo
alitoa takwimu za kunihusu ambazo siyo sahihi.
6. Ukweli ni kwamba mimi ninamiliki kwa ubia na
Watanzania wenzangu mgodi mmoja wa uchimbaji wa madini ya Tanzanite wenye eneo
lisilofikia hata kilomita mojaya mraba na siyo Dar es Salaam 3 kama alivyosema.
7. Naomba
nisisitize kwamba mimi binafsi nimeshapata nafasi kubwa ya kujiendeleza
kibiashara. Ukweli ni kwamba ninachopigania leo ni juhudi ya kupanua wigo ili
Watanzania wengi waweze kushiriki kama ilivyo kwenye Sheria ya Taifa ya Uwezeshaji Kiuchumi ya mwaka 2004,
(National Economic Empowerment Act, 2004) ambayo inatoa upendeleo maalumu kwa
Watanzania katika rasilimali zao.
8. Ninamatumaini makubwa kwamba katika mkutano wa kesho ambao
utatoa fursa kwa sekta binafsi kuzungumza na uongozi wa Taifa chini ya uwenyekiti
wa Mhe. Rais utatuwezesha kupata muafaka wa ni jinsi gani tutashirikiana katika
juhudi za kuwawezesha Watanzania kwenye nyanja mbalimbali za uchumi wetu.
Dkt. Reginald A.
Mengi
Dar es Salaam
0 comments:
Post a Comment