Mei 15, 2013 Dar es Salaam,
Jumatano iliyopita kupitia televisheni za ITV na Clouds TV timu ya Ghana
iliyoshinda katika kipindi cha Tisa cha GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE
walifurahia kupata nafasi katika nusu fainali kwa kucheza azonto ambayo
iliwafanya watangazaji Larry na Mimi kujiunga nao. Kofi Okarku na Isaac Aryee ingawa
hawakufanya vizuri katika hatua ya mwisho ya ukuta wa pesa wa Guinness
walifanikiwa kupata dola za kimarekani 1,500 na waliufanya uwanja
wote kunyanyuka na kucheza.
Timu iliyoshinda ilifanya vizuri katika hatua za mwanzo na kujipatia
alama 16 pamoja na kuonesha uwezo mzuri ufahamu wa soka. Waliwashinda Wakenya
katika hatua ya penati, hata hivyo timu ya Kenya imefuzu nusu fainali kama
washindi wa pili.
Emanuel, Kenneth, Chris na Isaac wataendelea kuziwakilisha nchi zao
katika hatua ya nusu fainali, wakiwa na ndoto za kufanya vizuri na kuwa washindi wa Pan-African Guinness Football
Challenge.
Meneja wa kinywaji cha Guinness Davis Kambi alisema, “Nusu fainali ya
kwanza inatarajia kufanyika wiki ijayo tukisubiri kuona ni nani atakayefanikiwa
kutinga fainali ya GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE. Timu kutoka
Dar-es-Salaam,Daniel Msekwa na Mwalimu Akida Hamad watapeperusha bendera ya
taifa letu na kuwakilisha Afrika mashariki hivyo tunawatakia kila la heri. Tunazisifu timu zote
na sasa timu bora zitakutana kuwania kufuzu kuingia fainali”
Timu zitakazoendelea na michuano ni pamoja na;
KWA WATANZANIA NDANI YA JEZI ZA KIJANI-Kutoka Dar-es-Salaam, Daniel Msekwa na Mwalimu Akida Hamad ambao
awali walijishindia dola za kimarekani 5,500 katika mashindano ya kitaifa na
waliishia katika hatua ya penati kwenye robo fainali wataweza kufikia hatua ya
pesa ukutani katika nusu fainali?
KWA WAKENYA
NYEUSI-Kenneth
Kamau na Wills Ogutu wote kutoka Nairobi.Ken ni kocha na Wills ni dereva.Timu
hii ilijishinda katika robo fainali ya pili na kuongeza dola 1,500 kwenye dola 3,000 walizokuwa nazo
awali.
JEZI NYEKUNDU-ni timu ya pili kutoka Kenya,Francis Ngigi kutoka Nairobi na Kepha
Kimani kutoka Thika.Timu hii ilipata dola 3,000 katika hatua za kitaifa na
walifika hatua ya penati katika robo fainali.
KWA WAGHANA
JEZI ZA BLU- Timu ya Ghana iliyopata fedha nyingi zaidi katika hatua ya kitaifa,
Jonathan Naab kutoka Tindogo na Desmond Odaano kutoka Larteh wamefanikiwa
kufika hatua ya nusu fainali baada ya kupata jumla ya dola 8,500. Je,
watafanikiwa kuingia fainali?
Nusu fainali ya kwanzaitarushwa na televisheni za ITV na Clouds TV usikose
kuangalia mchezo huu na kushangilia timu yetu.
Wapenzi wa kipindi hiki cha
Guinness football challenge nchini wanaweza kupima maarifa yao katika soka kupitia GUINNESS® VIP™. Wanaweza
kufanya hivyo kwa kujisajili bure kabisa katika m.guinnessvip.com
kwa kupitia simu ya mkononi.
Usikose
kuufwatilia ukurasa wa facebook wa GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE kwa habari
mbalimbali.
-www.facebook.com/guinnesstanzania
GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni
kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya
Endemol. Usikose kuangalia na
kufuatialia kipindi hiki katika runinga yako kupitia televisheni za ITV na
Clouds TV kila siku ya Jumatano usiku saa 3:15 ITV na saa 2:15 Clouds TV.
Usisahau kuwa na chupa ya bia
uipendayo ya Guiness wakati unaangalia kipindi hiki.
Tafadhali kunywa kistaarabu- Hairuhusiwi kuuzwa kwa wale wenye umri
chini ya miaka 18.
0 comments:
Post a Comment