ALIYEKUWA
mshiriki namba 6 katika shindano la kumsaka Redds Miss Kibaha 2013
Nzera Kitano ameibuka kua Redds Miss Kibaha 2013 katika shindano
lililofanyika kwenye ukumbi wa Conteainer Kibaha Maili Moja mkoani
Pwani.
Nzera
ambae alionekana kuwa mchezi tangu mwanzo wa shindano aliweza kupenya
katika hatua ya nusu fainali ambapo aliingia katika warembo watano bora
kati ya washiriki 10 waliokuwa wakishindana kuwania taji hilo.
Aidha
kwa ushindi huo Nzera amepata zawadi ya fedha taslimu sh.300,000 pia
amepa ofa ya kwenda kuchagua vipodozi na mapambo ya aina mbalimbali
katika duka la Shear Illusion lilipo Mlimani City pamoja na king’amuzi
kutoka kampuni ya Multichoice ambapo atafungiwa bure.
Mshindi
wa pili ni Ester Albert ambaye amepata fedha taslimu kiasi cha
sh.200,000 pia atapata ofa ya kulipiwa ada ya shule au kutafutiwa kazi
na mdau ambaye hataki kutaja kwenye vyombo vya habari.
Mshindi
wa tatu ni Rachel John aliyepata fedha taslimu sh. 150,000 huku nafasi
ya nne ikienda kwa Sylvia John huku nafasi ya tano ilikwenda kwa
Beatrice Bahaya.
Kwa
ushindi huo warembo wote watano wamepata nafasi ya kwenda kushiriki
kwenye shindano la Redds Miss Pwani watakakochuana na warembo wa
Bagamoyo kuwania tiketi ya kwenda kushiriki katika shindano la Kanda
ikiwa ni katika kuwania tiketi ya shindano la taifa.
Shindano
hilo limeandaliwa na Kampuni ya Linda Media Solution (LIMSO) na
kudhaminiwa na
Redds Miss Kibaha ilidhaminiwa na Tanzania Distilleries Konyagi kupitia
kinywaji cha Dododma Wine, Redds Premium Cold, Fredito Entertainment,
CXC Africa, Michuzi Media Group |(MMG), Aco Catering & Servises, Pr
Studio, ASET ,Santorine Holiday Resort na Amazon Night Club.
Bendi ya Muziki wa dansi ya Mashujaa ilitumbuiza na kuwachengua mashabi wa urembo wa mkoa wa Pwani.
0 comments:
Post a Comment